Thursday, November 6, 2014

PATRICK LIEWIG KOCHA MPYA AZAM KUTUA DAR NOVEMBA 17 KUANZA KAZI AZAM FC DAR





Kocha Patrick Liewig amekubaliana kila kitu na uongozi wa Azam FC na anatarajia kutua nchini Novemba 17, mwaka huu.

Azam FC imeamua kuboresha benchi lake la ufundi baada ya kuondokewa na kocha wake Vivek Nagul ambaye amepata ulaji kwao India.

Liewig raia wa Ufaransa anatarajia kutua nchini na ndege ya Shirika la Ndege la Qatar akitokea kwao Ufaransa.

Habari za uhakika kutoka kwa rafiki wa Liewig aishiye katika jiji la Paris, Ufaransa amesema kocha huyo amemhakikishia kuwa anakuja nchini.

“Nilikuwa na Liewig siku tatu zilizopita, amesema anakuja huko kwenu (Tanzania) kufanya kazi katika klabu inaitwa Azam FC. Wamekubaliana kila kitu na Novemba 17 atakuwa Dar es Salaam.

“Amesema anakuja kufundisha timu ya vijana lakini anaweza kutoa ushauri kwa timu ya wakubwa na mambo mengine lakini kikubwa kwake ni kuwakuza vijana,” kilieleza chanzo.

Chanzo hicho kimeeleza, Liewig angeweza kutua nchini mapema lakini alikwama kutokana na mkewe kuwa mgonjwa.

“Kweli mkewe alikuwa mgonjwa, tulikwenda kumuona kwa kuwa hapa (Paris) hadi kwake ni kama maili 30 hivi.”

Liewig alikuwa kocha wa Simba msimu uliopita. Lakini uongozi wa Ismail Aden Rage ukamuondoa na nafasi yake ukampa Abdallah Kibadeni ambaye hata hivyo hakudumu zaidi ya nusu msimu.

0 Responses to “PATRICK LIEWIG KOCHA MPYA AZAM KUTUA DAR NOVEMBA 17 KUANZA KAZI AZAM FC DAR”

Post a Comment

More to Read