Tuesday, January 13, 2015
EXCLUSIVE:: ABIRIA WA FASTJET WAKWAMA UWANJA WA NDEGE MBEYA.
Do you like this story?
Foleni ya mabegi hakuna wa kukagua kazi ipo jee huu ni uungwana? kuwasotesha Abiria namna hii? |
Na
Mwandishi Wetu, Mbeya.
KUFUATIA
kwa tatizo la kuchafuka kwa hali ya hewa iliyoambatamna na ukungu,
iliyojitokeza jJijini Mbeya jana hivyuo kusababisha ndege ya abiria ya Fastjet
kushindwa kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Songwe, leo abiria wamejikuta
wakipanga foleni ndefu ya kuingia ndani ya uwanja hali ambayo imeonekana
kuwakera baadhi ya wasafiri.
Mbali na
kero hiyo, pia wasafiri walilazimika kuwahi kufika kwenye uwanja huo na
kukaguliwa mapema ili kuondokana na hali ya usumbufu wakati wa kuingia ndani ya
uwanja huo.
Fahari
News, imeshuhudia foleni ndefu ya habaria wakiwa wanasubili kuingia kwenye
chumba cha ukaguzi huku baadhi yao wakionekana kukerwa na hali hiyo.
“Hii sasa
imekuwa shida kwani mtu umefika mapema lakini mpaka sasa tupo kwenye
foleni ambayo haieleweki itamalizika muda gani,” alisema abiria ambaye
ahakutaka jina lake liandikwe.
Amesema,
ikumbukwe kwamba abiria huwa anawahi kufika uwanjani ili kukamilisha taratibu
mapema na kupumzika lakini sasa angalia foleni ni ndefu na mtu anaweza jikuta
akichoka kabla ya kuanza safari ni vema serikali ikaharakisha mpango wa
ufungaji wa Taa kwenye uwanja huo.
“Kama Taa
zingekuwepo abiria ambao walipaswa kusafiri jana asubuhi na mchana wangeondoka
usiku wa saa nne hivyo kupunguza msongamano uliojitokeza hivi leo.”amesema
Aidha,
akizungumzia hilo, Mratibu wa shughuli za ndege Kampuni ya Fastjet Mkoa wa
Mbeya, Omary Idrissa, alikiri kujitokeza kwa msongamano mkubwa uwanjani lakini
suala hilo limerekebishika kwa kuwaomba abiria ambao walipaswa kuondoka na
ndege ya jana kuondoka kesho.
“Mpaka
sasa tumeweza kulitatua tatizo hili kwani baadhi ya abiria wameondoka na ndege
ya asubuhi wengine wataondoka leo jioni na wale ambao walitakiwa kuondoka jana
watatarajia kuondoka kesho kwani waliobaki ni wachache ,”amesema.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “EXCLUSIVE:: ABIRIA WA FASTJET WAKWAMA UWANJA WA NDEGE MBEYA.”
Post a Comment