Tuesday, January 20, 2015
WAFANYABIASHARA MBEYA WAZUA TAFRANI, WAANDAMANA MAHAKAMANI.
Do you like this story?
Mmoja wa viongozi wa wafanyabiashara
hao Ndugu Charles Syonga akizungumza na wafanyabiashara hao mara baada ya
kumaliza mazungumzo na uongozi wa mkoa juu ya kumaliza tatizo
|
Jeshi la Polisi likiimalisha ulinzi
katika eneo hilo(Picha na Fahari news)
|
(Fahari news)
MWENYEKITI wa Soko la Soweto jijini
Mbeya, Honola
Mbogella, amefikishwakatika mahakama ya Mwanzo Mbeya
mjinikwa tuhuma za kuzuia watumishi wa umma kufanya kazi zao. Kufuatia
kukamatwa kwaMwenyekiti huyo kulisababisha zaidi yawafanyabiashara 1000 wanaondesha
shughuli zao za kibiashara katika masokomatano yaliyopo Jijini Mbeya,
kuandamana na kuizunguka mahakama ya
Mwanzo yaMbeya mjini, wakishinikiza mahakama hiyo kumuachia
huru. Mwenyekiti huyo,amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo yaMbeya
mjini, leo na kesi yake kusikilizwa majira ya saa tatu asubuhi ambapo
kesi hiyo ilivuta hisia za watukutokana na kundi hilo la wafanyabiashara
kuizunguka mahakama hiyo, huku jeshila polisi likilazimika kuimarisha
ulinzi. Akisomea mashitaka hayo Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya
mwanzo ya Mbeya MjiniUbaswege Mathew, karani wa Mahakama hiyo, Sioni Kasunga,
alisema mtuhumiwa huyoalifanya kosa hilo January 10 mwaka huu akiwa katika eneo
lake la kazi la Sokola Soweto lililopo Jijini Mbeya. Alisema, kwa mujibu wa kifungu kidogocha cha sheria namba 101(a) sura ya 288iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mtuhumiwa aliwazuia watumishi wa umma wahalmashauri ya Jiji la Mbeya kufanya kazi yao ya kukusanya ushuru.
Alisema, mtuhumiwa
aliwazuiawafanyabiashara hao kugoma kutozwaushuru wa shilingi 200 hadi
300 na halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa maelezokwamba licha ya
wafanyabiashara hao kulipiatozo hiyo kwa kipindi kirefu bado soko hilo
limeendelea kukithiri kwa uchafu. Aidha, kutokana na kosa hilo,Hakimu wa
mahakama hiyo, Ubaswege Mathew,baada ya kusikiliza maelezo hayo,alitoanafasi
kwa mtuhumiwa ambaye alikana shitaka hilo hivyo, hakimu kuhairisha kesihiyo
mpaka kesho(leo) na kwamba dhamana kwa mtuhumiwa ipo wazi.
amesema Wakati kesi hiyo
ikiendeleamahakamani hapo, umati mkubwa wa wafanyabiashara wanaoendesha
shughuli zaokatika masoko matano ya Soweto,Uyole, Mabatini, Sokomatola na
Uhindini ulijitokeza na kuizunguka mahakama hiyo kwa kile walichokidai
kwamba Mwenyekityi huyo ameonewa. Wakizungumza na Fahari news ,nje
ya mahakama, wafanyabiashara hao ambao waligoma kutaja majina yao, walisema wao
wamegoma kulipa ushuru huo kutokana na halmashauri kushindwa kuetekeleza majukumu
yao ya ukarabati wa miundombinu pamoja na usafi wa mazingira hivyo Mwenyekiti
huyo hausiki na suala lakuwashawishi kugoma kama inavyodaiwa na
halmashauri. Hata hivyo, wafanyabiashara haowamegoma kuendelea na
shughuli zao mpaka suala hilo litakapo patiwa ufumbuzikwa halmashauri
kurekebisha miundombinu na usafi wa mazingira katika maeneo
yabiashara.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAFANYABIASHARA MBEYA WAZUA TAFRANI, WAANDAMANA MAHAKAMANI.”
Post a Comment