Tuesday, January 20, 2015
AJALI MBAYA DAR ES SALAAM, 40 WANUSURIKA KIFO.
Do you like this story?
Zaidi ya
watu arobaini wamenusurika kifo huku mmoja akikatika viungo vya miguu na
wengine kujeruhika vibaya baada ya lori moja lilionekana kuwa ni la jeshi
kugongana uso kwa uso na gari la abiria aina ya COSTA la ubungo Tegeta eneo la
Tegeta jijini Dar es salaam.
FAHARI NEWS imeshuhudia
tukio hilo lililovuta hisia za mamia ya wakazi wa Tegeta huku baadhi ya mafundi
gerejji wa Tegeta wakijaribu kutumia vifaa maalumu kukata mabati ya magari kwa
nia ya kunasua baadhi ya majeruhi walionasa ndani ya COASTA hiyo kusuru abiria
walioonekana kunasa katika vyuma vya magari hayo baadhi ya wamashuhuda na
Dereva wa COSTA pamoja na kuomba eneo la kibaoni kuweka njia ya mzunguko
maarufu kama ROUND ABOUT kwa lengo la kuepusha madereva wanao lazimika kugeuza
kwa dharura katika njia kuu maarufu kama UTAN kutokana na njia hiyo kukosa
fursa ya kugeuza endapo kuna ulazima wa kufanya hivyo pia wamemtupia lawama
Dereva wa Lori kama msababisha ajali kwa kukosa hekima ya kuchukua tahadhari kabla
ya kufanya hivyo.
Kamanda wa
polisi mkoa kipolisi kinondoni Kamilius wambura amethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo akieleza kutoa taarifa mara baada ya uchunguzi kufanyika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AJALI MBAYA DAR ES SALAAM, 40 WANUSURIKA KIFO.”
Post a Comment