Wednesday, January 21, 2015

WANAHABARI NCHINI KUALIKWA KUJIFUNZA ATHARI ZA VITA SUDANI KUSINI.




Na Gladness Mushi-Ngurudoto Arusha

 Waandishi wa habari kutoka katika
vyombo mbalimbali nchini Tanzania wanatarajiwa kuipelekwa nchini Sudan
Kusini ili kujifunza athari za vita ambazo zimetokea katika nchi ya
Sudani kusini.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu
mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana,leo wakati
akizungumza na waaandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini  baina
ya vikundi vinavyogombana kutoka nchini Sudani.

Kinana amesema kuwa baada ya
kuwekeana saini na makubaliano ya kuacha mapigano basi Nchi ya Tanzania
itachukua jukumu la kupekeka waaandishi wa habari Sudani kwa malengo  ya
kujifunza na kujionea athari za vita .
“Tunataka waandishi wetu wa habari kutoka Tanzania wapate  uelewa wa kutosha katika kuandika na kutangaza madhara
vita vya wenyewe kwa wenyewe, Kinana aliahidi kuwa ni muhimu na atahakikisha

anawapeleka waandishi wa habari  waitembelee Sudan Kusini,”alisema.
Kinana alifafanua kuwa yeye binafsi anaamini watakapokwenda kujionea kwa macho madhara ya vita

wataweza kutumia vema kalamu zao kuelimisha watanzani

Chama Cha Mapinduzi (CCM)

kiliombwa kufanya na kusimamia mazungumzo juu ya vita hiyo na ndivyo watakavyofanya
pia kwa waandishi ili wapate somo.
Alisema mapigano hayo yamesababisha uchumi wa nchi hiyo kurudi nyuma
ukizingatia kuwa wao ni wazalishaji wakubwa wa ng’ombea na watatu

katika nchi za Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo ambapo pia wana utajiri mkubwa wa mafuta.

alisema Sudan Kusini ilihangaika miaka zaidi ya 50 kutafuta uhuru wao, miaka
miwili baada ya kujitenga kutoka Sudan Kaskazini, baada ya asilimia
90% kupiga kura ya kujitenga wakaanza vita ya kugombea madaraka, sasa
kila familia imeathirika kutokana vita ndio wanasaka amani.
Mazungumzo ya kutafuta amani kwa nchi hiyo yalianza mapema Desemba 23
na 24 mwaka jana 2014 katika Hotel ya Ngurudoto, Wilayani Arumeru,
Mkoan Arusha, huku zikiwakutanisha pande zote tatu zinazopigana kwa

ajili ya kusaka madaraka
Katika mazungumzo hayo mwenyekiti wa mazungumzo hayo ni Balozi Dk.

John Samwel Malecela, ambaye pia alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu awamu

ya pili ya uongozi wa Rais Ally Hassan Mwinyi
Mapigano hayo ya ndani ya chama cha SPLM katika nchi ya Sudani Kusini

yanahusisha makundi matatu ambapo kila kundi linataka madaraka ya

kuongoza nchi hiyo.

0 Responses to “WANAHABARI NCHINI KUALIKWA KUJIFUNZA ATHARI ZA VITA SUDANI KUSINI.”

Post a Comment

More to Read