Wednesday, January 21, 2015

SHUGULI ZA BIASHARA ARUSHA ZASIMAMA KWA SABABU YA MGOMO.




Shuguli mbalimbali ndani ya jiji la Arusha zikiwemo za kibiashara jana(leo)zimelazimika kusimama mara baada ya mabasi ya abiria (Daladala) kugoma kubeba abiria kwa madai kuwa utaratibu wa Ruti ndefu zilizopangwa na Sumatra ni uonevu mkubwa

hataivyo kugoma kwa daladala hizo pia kuliweza kuwaaathiri wanafunzi ambao wanatumia usafiri huo kwa ajili ya kwenda mashuleni hali ambayo iliwafanya wakose masomo lakini pia baadhi yao wafike mashuleni wakiwa wamechelewa.

Akiongea kwa niaba ya madereva daladala ambao wamegoma dereva,Jumaa isa alisema kuwa wanashangazwa sana na Sumatra kuweza kuwapangia Ruti ndefu wakati bado hata abiria wa Jiji la Arusha hawana uwezo wa kutumia hizo ruti ndefu.

Jumaa alisema kuwa kwa historia ya mji wa Arusha abiria wanakuwepo majira ya asubui na jioni kwa pekee ila kwa majira ya mchana abiria ni wachache sana sasa hali hiyo inafanya mparangano mkubwa sana barabarani.


aliendelea kwa kusema kuwa hapo awali kulikuwa na vikao ambavyo vilifanyika lakini hakuweza kukubalina muafaka wa ruti ndefu ambazo Sumatra walikuwa wanazitaka kitu cha kushangaza ni kwamba tayari wameshaambiwa kuanza ruti ndefu jambo ambalo wamelipinga.


katika hatua nyingine akiongea kwa niaba ya abiria Bi Neema Palangyo kutoka katika eneo la kwa Muorombo alisema kuwa mgomo huo umesababisha madhara makubwa sana kwa wananchi wa Arusha kwani uzalishaji wa siku hiyo ya mgomo ni mkubwa sana.


Hataivyo zaidi ya daladala mia tano ambazo zote zinafanya shuguli zake za usafiri jijini Arusha ziliweza kugoma na kisha kupinga azimio hilo la ruti ndefu ambalo lilitolewa kwa kushirikiana na wadau wote wa Sumatra na usafirishaji Jijini Arusha.

0 Responses to “SHUGULI ZA BIASHARA ARUSHA ZASIMAMA KWA SABABU YA MGOMO.”

Post a Comment

More to Read