Monday, January 12, 2015
KOCHA MPYA SIMBA SC: NINAIOGOPA REAL MADRID, SIYO YANGA SC.
Do you like this story?
Na Bertha Lumala
Unajua alichokisema Mkuu mpya wa Simba
SC, Mserbia Goran Kopunovic baada ya kumzidi mjanja Mholanzi wa Yanga SC, Hans
van der Pluijm kwa kutinga fainali za michuano ya Kombe la Mapinduzi? Tega
sikio.
Baada ya kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi,
Kopunovic amesema hakuwa na hofu kukutana na Yanga SC katika michuano hiyo
inayofanyika kwa mara ya tisa tangu ianzishwe 2007.
Simba imefanikiwa kuifuata Mtibwa Sugar
FC fainali baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Zanzabar katika
mechi ya pili ya nusu-fainali iliyochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar jana usiku.
Mara tu baada ya mechi hiyo kumalizika
huku kiungo Said Hamis Ndemla wa Simba SC akitangazwa mchezaji bora wa mechi na
kukabidhiwa zawadi ya king'amuzi cha Azam FC, Kopunovic alipigwa swali na
waandishi kuhusu hofu yake juu ya kasi iliyooneshwa na wapinzani wao wa jadi
Yanga SC, lakini Mserbia huyo akasema kamwe hakukihofia kikosi hicho cha
Jangwani.
"Ha, ha, haah! Mimi? Niulizeni
swali jingine kama lipo. Ningelihofu ningeliambiwa Real Madrid inakuja
kushiriki mashindano haya, siyo Yanga. Hiyo Yanga haipo hata fainali kwa sasa.
Je, mechi ya fainali haitachezwa kwa sababu Yanga haipo?" Alihoji
Kopunovic aliyeiongoza Simba SC katika mechi nne akianza na mechi yao ya pili
ya Kundi C waliyoshinda bao 1-0 dhidi ya Mafunzo FC Januari 3.
Kocha huyo hakuwa benchini wakati
kikosi cha Msimbazi kikikung'utwa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar FC katika mechi yao
ya kwanza ya Kundi C. Kocha huyo alikuwa amekaa Jukwaa la VIP A la Uwanja wa
Amaan akiisoma timu ykae hiyo mpya.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Polisi
Zanzibar, Khamis Sufian alisema alikiandaa kikosi chake kucheza soka la
kujilinda weakitarajia matuta lakini kimeangushwa na kipa Mohamed Abdulrahim
aliyeshindwa kuokoa shuti la faulo la Ramadhani Singano 'Messi' lililokwenda
moja kwa moja langoni katika dakika ya 26.
Polisi ilifanikiwa kutinga hatua hiyo
baada ya kuwang'oa kwa matuta waliokuwa mabingwa watetesi KCCA ya Uganda wakati
Simba SC iliing'oa Taifa ya Jang'ombe kwa kipigo kibaya cha mabao 4-0 ikiwa ni
sawa na kipigo ilichokipokea kutoka kwa Yanga SC katika hatua ya makundi.
Bottom of Form
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KOCHA MPYA SIMBA SC: NINAIOGOPA REAL MADRID, SIYO YANGA SC.”
Post a Comment