Tuesday, January 27, 2015

MTIKILA AMSHITAKI MOKIWA, ADAI FIDIA YA SH BILIONI 1 KWA KUDHALILISHWA






Katika upekuzi huo ndipo tuhuma hizo zilipopatikana kutokana na madai kwamba operesheni hiyo ilienda mbali zaidi ya lengo la kawaida.

Wakili wa Upande wa mashtska aliiambia mahakama kuwa, "Mlalamikiwa alitangaza kuwa, kila mtu aliyekuwemo kwenye mkutano lazima apekuliwe na kwamba atakayekataa angetumia nguvu, kwa kuwa alikuwa na bastola, hakuna aliyebisha."

Alisema kisha akaendelea "Mshtakiwa (Mokiwa) alianza kupenyeza mikono yake kwenye shingo kuelekea chini kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa ilionekana waziwazi ikipapasa makalio ya mlalamikaji".

Mchungaji Mtikila ameiomba Mahakama imwamuru Askofu Mokiwa alipe fidia ya shs. bilioni moja kwa kumdhalilisha.

Madhara zaidi ya kitendo hicho ni pamoja na mfadhaiko, masikitiko, wasiwasi, aibu katika jamii na kupata shinikizao la damu la mara kwa mara na matatizo ya moyo kila anapokumbuka kitendo hicho.

Kesi inasikilizwa kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, chini ya Hakimu Agness Mchome.

Source:Sufianimafoto

0 Responses to “MTIKILA AMSHITAKI MOKIWA, ADAI FIDIA YA SH BILIONI 1 KWA KUDHALILISHWA”

Post a Comment

More to Read