Monday, January 26, 2015
RAIS MPYA WA ZAMBIA AVALISHWA NA MBUNIFU WA KITANZANIASHERIA NGOWI.
Do you like this story?
![]() |
Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akikagua gwaride rasmi kabla ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish |
![]() |
Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akila kiapo cha kuwa Rais Mpya wa Zambia katika sherehe za zilizofanyika jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish |
![]() |
Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akipokea salaam Maalum Kutoka kwa Rais wa Mpito wa Zambia Guy Scotts Muda mfupi baada ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. |
Mbunifu wa
mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ameendelea kuipeperusha bendera ya
Tanzania kupitia kipaji chake cha ubunifu wa mavazi baada ya kumvalisha
Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi
katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
Rais Lungu
58, aling’arisha sherehe hizo baada ya kuvaa suti rasmi (Presidential
suit) rangi ya bluu, shati jeupe na tai nyekundu zilizobuniwa na Mbunifu
wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi. Lungu aliambatana na mke wake,
Eshter Lungu walipokuwa wanaingia viwanjani hapo huku wakisindikizwa na
ulinzi mkali.
Akizungumza
baada ya hafla hiyo, Sheria Ngowi alisema amefurahi kupata nafasi ya
kipekee ya kumvalisha Rais Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake na
kusema ni hatua kubwa katika kazi yake kama mbunifu wa mavazi wa
kimataifa.
“Hii ni
hatua kubwa katika kazi yangu ya ubunifu wa mavazi, namshukuru Mungu
kwa kipaji alichonipa kinachoweza kunitambulisha na kunifanya niaminike
hata kufikia hatua ya kuvuka mipaka ya Tanzania na kumvalisha Rais mpya wa
Zambia, Mheshimiwa Edgar Lungu”, alisema Ngowi.
Mbunifu
Ngowi alisisitiza kuwa juhudi, nidhamu, bidii na kumweka Mungu mbele
ndio chachu ya mafanikio katika kila utendaji wa kazi zake akiwa na
malengo ya kuipeleka kazi yake katika nyanja za kimataifa hata kutambulika
katika sekta ya ubunifu wa mavazi duniani kote.
Hafla
hiyo ilihudhuriwa na aliyekuwa Rais wa muda wa Zambia, Guy Scott na
mke wake Charlotte, Mwenyekiti wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za
kusini(SADC), Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, baadhi ya viongozi wa juu wa
Zambaia na nchi mbalimbali pamoja na wananchi wake.
Mbunifu
huyo ameendelea kuonyesha na kudhihirisha kuwa Tanzania ni nchi yenye
vipaji vinavyoweza kuiletea nchi ya Tanzania sifa na kuinua uchumi wake
katika sekta mbalimbali. Hii si mara ya kwanza kwa mbunifu huyo kukata
mawingu kuitangaza nchi yetu, kwani ni miongoni mwa wabunifu mashuhuri
kutoka Afrika wanaopata fursa kuonyesha ubunifu
wa mavazi yao katika maonyesho ya kimataifa kama vile New York Fashion Week nchini Marekani na Mercedes Benz fashion Week nchini Afrika Kusini.
wa mavazi yao katika maonyesho ya kimataifa kama vile New York Fashion Week nchini Marekani na Mercedes Benz fashion Week nchini Afrika Kusini.
Hii ni
changamoto pia kwa wabunifu wa Tanzania kuziwania fursa zilizopo na
pia kuongeza juhudi ili kutangaza na kupeleka kazi zao katika soko la
kimataifa kama vile Sheria Ngowi alivyofungua mlango.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RAIS MPYA WA ZAMBIA AVALISHWA NA MBUNIFU WA KITANZANIASHERIA NGOWI.”
Post a Comment