Friday, July 24, 2015
VITUKO VYATAWALA MCHAKATO WA KUWANIA UBUNGE NDANI YA CHAMA JIMBO LA MBEYA MJINI.
Do you like this story?
MWENYEKITI wa UVCCM mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna, naye akipiga magoti kuomba kura |
MWENYEKITI wa Jumuia ya Wazazi ya CCM mkoa wa Mbeya, Fatuma Kasenga
akiomba kura
|
Hayo yalijiri wakati makada hao, wanaowania kuomba kuteuliwa na CCM wilaya ya Mbeya mjini, walipokuwa wakijinadi kwa wana-CCM wa kata ya Nsalagha,ili kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuipeperusha bendera ya CCM.
Vituko
hivyo vilileta bashasha na burudani ndani ya kata hiyo, na kuwafanya baadhi ya
viongozi waliokuwa meza kuu kulazimika kusimama ili kwenda kumuinua Mwenyekiti
wa Jumuia ya Wazazi mkoani hapa, Fatuma Kasenga, aliyekuwa anagalagala ardhini
kuomba kura.
Aliongeza lengo la kujitokeza kuwania nafasi hiyo ni
kutaka kurudisha heshima ya jimbo la Mbeya, ambayo hivi sasa imepotea baada ya
jimbo hilo kuwa chini ya mbunge wa kutoka chama cha upinzani kwa miaka mitano
sasa.
Fatuma ambaye alikuwa
akijinadi huku akiwa amepiga magoti, ambapo mara baada ya kumaliza dakika zake
tatu alizokuwa amepewa pamoja na kujibu maswali aliyoulizwa, ndipo alipoanza
kugalagala huku akiomba kura kwa wana-CCM.
Hatua hiyo iliwafanya
baadhi ya viongozi waliokuwa meza kuu, kulazimika kusimama na kwenda kumsaidia
kumuinua kasha kumsindikiza walipokuwa wamepangiwa kukaa wagombea wenzake.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM
mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna, alisema wakati anachaguliwa kushika nafasi hiyo
mwaka 2012, alikuta asilimia kubwa ya vijana ndani ya jiji la Mbeya wakiwa
wamekata tamaa na kuhamia upinzani.
Mara baada ya kumaliza kujinadi kwa wana-CCM hao, Kajuna aliamua kupiga magoti na kuomba kura akiwaahidi wanachama hao kuwa anao uhakika wa asilimia nyingi kuwa anao uwezo wa kulikomboa jimbo hili, kwani ametoa misaada mingi kwa vijana, wanawake na wazee.
Makombe
alisema akipewa ridhaa hiyo anao uhakika wa kulikomboa jimbo la Mbeya mjini, na
baada ya kutekeleza hilo atahakikisha anatafuta wafadhiri watakaojenga viwanda
ili viweze kutoa ajira kwa vijana mjini Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “VITUKO VYATAWALA MCHAKATO WA KUWANIA UBUNGE NDANI YA CHAMA JIMBO LA MBEYA MJINI.”
Post a Comment