Monday, August 31, 2015
-MGOMBEA WA CCM AFARIKI DUNIA BAADA YA KUZINDUA KAMPENI.
Do you like this story?
Mgombea
udiwani wa Kata ya Bomang’ombe wilayani Hai kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), Livingstone Nkya maarufu kama Ferefere, amefariki
dunia ghafla muda mfupi baada ya kuzindua kampeni zake za kuwania nafasi hiyo.
Ferefere
alifariki jana jioni baada ya kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya
mjini Moshi, kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Katibu
wa CCM Wilaya ya Hai, Allan Kingazi, alilithibitishia Nipashe kwa njia ya simu
jana kuwa, mgombea huyo aliaga dunia baada ya kuzindua kampeni za uchaguzi
kwenye kata hiyo.
Alisema
Ferefere alianza kuhisi afya yake inabadilika na kumfanya kushindwa kuendelea
na jukumu la kujieleza, hivyo aliamua kuondoka baada ya mkutano huo na kwenda
kutibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi, kabla ya
kuhamishiwa KCMC.
Kata
ya Bomang’ombe ni miongoni mwa kata mpya tatu zilizogawanywa katika Jimbo la
Hai, lililokuwa likiwakilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.
“Ni
kweli mgombea wetu amefariki jana usiku katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC
majira ya jioni; na hivi sasa tuko kwenye taratibu za kuandaa mazishi yake.
Tunasubiri majibu ya daktari kujua amefariki dunia kutokana na tatizo gani,
lakini sisi kama CCM tutasimamisha mgombea mwingine ili kutwaa kata hiyo,” Kingazi
Msimamizi
wa uchaguzi wa jimbo la Hai, Said Mderu alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi iwapo
uchaguzi huo utaahirishwa au laa, alisema,” Mimi sina taarifa za kifo hicho
na kwa sasa nipo njiani, siwezi kuzungumza lolote. Nitafute kesho (leo)
nitakuwa na majibu.
Ferefere
ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa maduka ya vileo na vinywaji baridi
mjini hapa, alikuwa akigombea kiti hicho, akishindana na mgombea wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joe Nkya ambaye
naye ni mfanyabiashara wa maduka ya pembejeo za kilimo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “-MGOMBEA WA CCM AFARIKI DUNIA BAADA YA KUZINDUA KAMPENI.”
Post a Comment