Saturday, May 21, 2016
. MAREKANI YATOA SALUTI KWA WAPIGANAJI WA TANZANIA… YAMTUNUKU NISHANI YA ULIPUAJI WA MIZINGA MEJA JENERALI JAMES MWAKIBOLWA
Do you like this story?
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Marekani linaloshughulikia masuala ya kijeshi barani Afrika,
Meja Jenerali Darrly Williams, amemtunuku mkuu wa majeshi ya vikosi vya nchi
kavu Tanzania Meja Jenerali James Mwakibolwa nishani ya ulipuaji bora wa
mizinga nchini.
Nishani
hiyo ambayo imekuwa ikitolewa na Rais wa Marekani, alitunukiwa Meja Jenerali
Mwakibolwa baada ya kuwa mstari wa mbele kurudisha amani kwenye nchi
zinazokabiliwa na vita barani Afrika.
Akizungumza
wakati wa kufunga mkutano wa wakuu makamandi wa vikosi vya nchi kavu barani
Afrika, uliofanyika mkoani Arusha, Jenerali Williams alisema jeshi la Marekani
barani Afrika, linamtambua Mwakibolwa kuwa mchapa kazi bora.
“Mwakibolwa
ni mtaalamu sana kwenye masuala ya mizinga, hata tulipokwenda kwenye mafunzo ya
kijeshi katika kambi ya Monduli, tumeona umahiri wake na tuzo hii anastahili
kwa kuwa anafanya vizuri.
“Jeshi
la Tanzania limekuwa mstari wa mbele kutoa kikundi cha M23 kwenye nchi ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na yote hayo ni kutokana na uchapakazi
wa Jenerali Mwakibolwa,” alisema
Jenerali Williams.
Akitoa
maoni yake kuhusu tuzo hiyo, Jenerali Mwakibolwa aliahidi kuhakikisha Jeshi la
Tanzania linakuwa imara zadi barani Afrika.
Alisema
Tanzania inazingatia masuala ya kijinsia katika jeshi hilo na sasa asilimia 25
ya wanajeshi ni wanawake.
“Jeshi
la Tanzania tuna wanawake wenye vyeo vikubwa na wako ambao tumewapa kazi kwenye
idara mbalimbali. Tunaamini mwanamke anaweza,” alisema Jenerali Mwakibolwa.
Kuhusu
maazimio ya mkutano huo, alisema wanaangalia namna ya kutoa mafunzo ya
kupambana na ugaidi wa baadhi ya wanajeshi wa Afrika.
Naibu
Katibu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Tanzania, Immaculate Ngwale alisema
mkutano huo umekuwa na faida kwa kuwajengea uimara askari wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “. MAREKANI YATOA SALUTI KWA WAPIGANAJI WA TANZANIA… YAMTUNUKU NISHANI YA ULIPUAJI WA MIZINGA MEJA JENERALI JAMES MWAKIBOLWA”
Post a Comment