Friday, May 20, 2016
MKAPA KUONGOZA TIMU YA USULUHISHI WA MGOGORO WA BURUNDI
Do you like this story?
Rais Mstaafu wa Awamu
ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Benjamin Mkapa,
ameteuliwa kuongoza mazungumzo kuhusu mgogoro wa Burundi ikiwa ni jitihada za
viongozi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika kuleta amani ya kudumu
nchini humo.
Mheshimiwa Mkapa,
aliyeteuliwa na Mkutano wa 17 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki atakuwa kiongozi wa timu ya usuluhishi wa mgogoro wa Burundi katika
kikao kitakachofanyika kuanzia mei 21 hadi 24 mwaka huu, katika ukumbi wa
mikutano wa Kimataifa ulipo jijini Arusha (AICC), ambapo inatazamiwa wadau wa
pande zote za mgogoro watashiriki.
Aidha, Mkutano huo wa
17 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ulifafanua kuwa
Rais wa Uganda, Mheshimiwa Yoweri Museveni, ataendelea kuwa msuluhishi wa
kudumu kutoka jumuiya hiyo.
Serikali ya Burundi
ilikubali kufanyika usuluhishi na iko tayari kushiriki katika mazungumzo ya
amani yanayofanywa na viongozi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki yakihusisha
wadau wote wa siasa nchini Burundi ikiwa ni jitihada za kuumaliza mgogoro wa
kisiasa unaoendelea nchini humo.
Imeandikwa na
Immaculate Makilika- MAELEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MKAPA KUONGOZA TIMU YA USULUHISHI WA MGOGORO WA BURUNDI”
Post a Comment