Monday, June 6, 2016

YANGA YAMSAINISHA MIAKA MIWILI KIPA WA PRISOSN




KIPA wa Prisons  Benno Kakolanya amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na wafalme wa soka ya Tanzania, Yanga SC.

Usajili huo ni pigo kwa Simba SC ambao pia walikuwa wanamtaka kipa huyo, lakini ‘Chelewa Chelewa, mwana si wao tena” – kwani wenye kisu kikali wamefanya yao. 

Akizungumza  leo Kakolanya amesema kwamba amesaini Yanga baada ya kumaliza Mkataba wake wa miaka mitatu Prisons ya Mbeya.

“Nimesaini miaka miwili kujiunga na Yanga, baada ya kumaliza Mkataba wangu Prsons,”amesema kakolanya ambaye ni kipa wa tatu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kakolanya sasa anakwenda kuungana na makipa watatu waliopo Yanga, Deo Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Benedicto Tinocco kufanya idadi ya makipa wanne.

Hata hivyo, mustakabali wa Tinocco haueleweki sasa baada ya kusajiliwa kwa Kakolanya mwenye umri wa miaka 22, ambaye Prisons ilimuibua Mbaspo Academy.

0 Responses to “YANGA YAMSAINISHA MIAKA MIWILI KIPA WA PRISOSN”

Post a Comment

More to Read