Monday, July 18, 2016
DEREVA MAARUFU WA MBIO ZA MAGARI AFRIKA KUSINI GUGU ZULU AFARIKI AKIPANDA MLIMA KILIMANJARO
Do you like this story?
Gugu Zulu akiwa na mke wake |
Kifo
chake kimethibitishwa na taasisi ya Nelson Mandela iliyokuwa imeandaa upandaji
huo wa mlima Kilimanjaro ujulikanao kwa jina la Trek4Mandela. Zulu alikuwa
sehemu ya kundi la waafrika Kusini wengine waliokuwa wakipanda mlima huo
akiwemo mke wake, Letshego Zulu.
Taasisi
hiyo imedai kuwa Zulu amefariki Jumatatu hii wakati akijaribu kufika kwenye
kilele cha mlima huo. Inadaiwa kuwa Gugu alipata shida ya kupumua na watu wa
huduma ya dharura walimwekea drip na kushuka naye.
“I am
devastated. I knew him well. I recruited him to climb Kilimanjaro. The last
thing he said to me at the airport before he left last week was that he wanted
to speak about doing other Mandela Day projects. I feel a huge sense of loss, ”
amesema mwenyekiti mtendaji wa taasisi hiyo, Sello Hatang.
Picha
ya mwisho aliyoweka kwenye Instagram ilikuwa jana Jumapili.
“Acclimatization
day3 – just taking a stroll in the garden high above a blanket of clouds –
amazing #Trek4Mandela #AdventureLiving,” aliandika.
Jumamosi
pia alipost nyingine inayomuonesha akiwa na mke wake na kuandika:
Made
it though day2. My wife is doing fabulous, she has even learnt the local
language. Am having flu like symptoms and struggling with the mountain but
taking it step by step!! Today we managed to see our destination and our camp
is literary above the clouds!! Bring day 3.”
Zulu
alikuwa dereva wa mbio za magari mwenye mashabiki wengi na alikuwa akiendesha
magari ya Volkswagen. Ameacha mke na mtoto wa kike mwenye mwaka mmoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DEREVA MAARUFU WA MBIO ZA MAGARI AFRIKA KUSINI GUGU ZULU AFARIKI AKIPANDA MLIMA KILIMANJARO”
Post a Comment