Monday, July 18, 2016
RAIS MAGUFULI ATEMA CHECHE WAKATI AKIWAAPISHA MAKAMISHINA WA POLISI WALIOPANDA VYEO
Do you like this story?
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Makamishna
Wasaidizi Waandimizi na Mananibu Kamishna wa Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa
bidii zote bila ya kumuogopa mtu yeyote katika kuhakikisha maslahi ya nchi
yanawekwa mbele.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwaapisha
wa umma waliopandishwa vyeo hivi karibuni na Rais mwenyewe kutoka
Makamishna Wasaidizi kuwa Makamisha Wasaidizi Waandamizi na waliokuwa
Makamishna Wasaidizi Waandimizi kuwa Manaibu Kamishna Wasaidizi.
Amewataka
watumishi hao wa umma kufanya kazi kwa moyo mmoja na kutenda haki kwa watu bila
kujali cheo wala umaarufu wa watu.
Akitolea
mfano wa Askari wa Usalama barabarani Rais Magufuli amesema wamekuwa
wakishindwa kukamata baadhi ya magari yanayomilikiwa na baadhi ya polisi
kama Happy Nation na Buffalo pale yanapofanya makosa na pindi wanapochukua
hatua dhidi ya magari ya aina hiyo basi wanatishiwa kushushwa cheo au
kuhamishwa kutoka pale walipo.
"Nataka
mkafanye kazi kwa haki bila kuogopa mtu hata kama ni gari la IGP, Waziri au
hata Rais sheria lazima ichukue mkondo wake na mhusika wa gari hilo atakwenda
kujieleza polisi mwenyewe." amesema
Rais Magufuli
Rais
Magufuli amewataka makamishna hao waliopandishwa vyeo kuhakikisha sekta zote
zinazotakiwa kulipa kodi kama bandari na utalii zinafanya hivyo kama sheria
inavyosema huku akiwashangaa wale wanaosema kuwa meli zimepungua bandarini na
watalii kupungua nchini.
“Meli
zilizopungua bandarini ni zile ambazo zimekuwa hazilipi kodi kwakuwa sasa
mianya yote ya kukwepa kodi imezibwa. Ni afadhali zile meli chache zitakazolipa
kodi kuliko nyingi ambazo hazilipi kodi na vivyo hivyo katika sekta ya utalii
ni bora watalii wasije kama hawataki kulipa VAT iliyotengwa na Serikali,” amesema Rais Magufuli.
Aidha,
amewataka makamishna hao kwenda kupambana na Tatizo la watumishi hewa katika
maeneo yao ya kazi ili kuhakikisha tatizo hilo ambalo limeigharimu serikali
mabilioni ya pesa halijirudii tena na kama bado lipo linatokomezwa kabisa.
Akiongelea
suala la Polisi Jamii, Rais Magufuli amewataka makamishna hao kufanya kazi bila
kujali utaratibu huo wa polisi jamii na kuongeza kuwa amekuwa akiupinga
utaratibu huo tangu akiwa Waziri wa Uvuvi na kusisitiza kuwa dunia ya sasa ni
tofauti na ile tuliyoizoea.
“Ilikuwa
unaweza kumkuta mvuvi katikati ya ziwa akiwa anafanya vitu kinyume na sheria
alafu unataka kuleta mambo ya polisi jamii kwa kuanzisha majadiliano na
mhalifu, hili halikubaliki na nililipinga kwani ni lazima ifike mahali polisi
aheshimiwe na tofauti iwepo kati ya polisi na raia wa kawaida,” amesisitiza Rais Magufuli.
Jumla ya
Makamishna Wasaidizi Waandimizi na Mananibu Kamishna 60 wa Jeshi la Polisi
wamepandishwa cheo na Rais Magufuli hivi karibuni na leo wamekula kiapo cha
uadilifu isipokuwa Manaibu Makamishna wawili ambao wapo nje ya nchi kwa mafunzo
maalum.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ RAIS MAGUFULI ATEMA CHECHE WAKATI AKIWAAPISHA MAKAMISHINA WA POLISI WALIOPANDA VYEO”
Post a Comment