Friday, July 8, 2016
MAJAMBAZI YATEKA KIJIJI KWA MASAA MATATU MKOANI KAGERA.
Do you like this story?
MAJAMBAZI
wanne wamevamia kijiji cha Benaco kilichopo katika Wilaya ya Ngara mkoani
Kagera kwa muda wa saa tatu ambapo wamefanikiwa kupora Sh milioni 2.4 na simu
ambazo hazikujulikana idadi yake kwa mfanyabiashara mmoja wa huduma ya M-Pesa.
Kaimu kamanda
wa polisi mkoa wa Kagera ambaye pia ni ofisa upelelezi wa polisi mkoa huo, Abel
Mtagwa, alisema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana ambapo
majambazi hao walikuwa na silaha moja ya kivita aina ya SMG.
Alisema
kuwa wakati majambazi wakijiandaa kuondoka eneo hilo walimpiga risasi
mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Gankabo Wilayani
Kibondo mkoani Kigoma aliyetambuliwa kwa jina la Nelson Simon (15) na kumjeruhi
mguu wake wa kulia. Mwanafunzi huo amelazwa katika hospitali teule ya Murgwanza
iliyopo wilayani humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAJAMBAZI YATEKA KIJIJI KWA MASAA MATATU MKOANI KAGERA.”
Post a Comment