Wednesday, July 20, 2016
MIKOA YA DAR ES SALAAM NA DODOMA YAONGOZA KWA MAPENZI YA JINSIA MOJA.
Do you like this story?
Takwimu zilizotolewa
na wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia , watoto na wazee nchini
zinaonyesha kuwa mkoa wa Dar es salaam na Dodoma inaongoza kwa vitendo vya
mapenzi ya jinsia moja
Akiongea
na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam waziri wa wizara hiyo Mhe.
Ummy Mwalimu alisema kutokana na hali hiyo wizara imepiga marufuku matumizi ya
vilainishi vinavyotumiwa na baadhi ya makundi yanayo jihusisha na vitendo
hivyo.
Mhe. Ummy
Mwalimu alisisitiza kuwa serikali imeamua kuzuia vilainishi hivyo kwani vimetajwa
kuchochea vitendo hivyo ambavyo nikinyume na sheria na taratibu za nchi
nakuongeza kuwa vitendo hivyo nimiongoni mwa sababu inayochangia ongezeko la
VVU.
Aidha Mhe.
Ummy alisema kuwa kwa sasa serikali inajikita kuhakikisha kuwa inajenga wodi za
wazai, kununua vifaa tiba, madawa ya kutosha katika hosptali zake na sio
ununuzi wa vilainishi hivyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MIKOA YA DAR ES SALAAM NA DODOMA YAONGOZA KWA MAPENZI YA JINSIA MOJA.”
Post a Comment