Monday, November 14, 2016
VYOO 100 KUJENGWA BARABARA YA MWANZA KWENDA DAR ES SALAAM
Do you like this story?
Taasisi
ya The Desk & Chair Foundation (TD& CF), inatarajia kujenga vyoo 100
katika Barabara Kuu ya Mwanza-Shinyanga-Dar es Salaam unaokadiriwa kutumia Sh. milioni
500.
Mwenyekiti
wa TD & CF, Alhaji Sibtain Meghjee alisema hivi karibuni mjini Mwanza
kwamba mradi huo ni sehemu ya miradi mitatu mikubwa ambayo taasisi yake
inatekeleza nchini.
Alisema
baada ya kukamilisha mradi mkubwa wa jengo la kupumzikia wananchi
wanaokwenda kutibiwa na kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure wanatarajia kujenga vyoo 100 kwenye
barabara ya kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kwa basi.
Meghjee
alieleza kuwa maandalizi ya awali ya mradi huo yameshaanza na kwamba
watashirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu
(SUMATRA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ili kupata taarifa sahihi
kabla ya mradi kuanza.
“Penye
nia pana njia, baada ya kukamilisha ndoto yetu, leo ya mradi huu mkubwa wa
ujenzi wa jengo la kupumzikia hapa Sekou Toure, tunatarajiwa kutekeleza miradi
mitatu mikubwa ukiwemo wa vyoo kwa ajili ya abiria wanaosafiri kati ya
Mwanza na Dar es Salaam:
“Tunataka
msamiati wa kuchimba dawa wakati wa safari ubaki kuwa historia kwa hiyo
tunatarajia kufanya jaribio moja la kujenga matundu 100 ya vyoo katika njia na
barabara kuu ya Mwanza hadi Dar es salaam ambavyo vitagharimu shilingi milioni
500.Tutashirikiana na mamlaka husika, ofisi yako na idara ya afya,”alisema Meghjee.
Meghjee
alieleza kuwa taasisi hiyo pia ina mpango wa kutekeleza mradi wa kutengeneza
viungo bandia kwa kushirikiana na kitengo cha Jairpur Foot/Knee and Limb
Project cha India ambao unahitaji Dola 200,000 za Marekani (sh. milioni 44),
zitakazowezesha kuanzisha huduma ya viungo hivyo bandia vya miguu, mikono,
fimbo na baiskeli.
Alisema
wanaendelea kuwasiliana na wafadhili watakaoshirikiana nao kwenye mradi huo na
kuwahakikishia walengwa kuwa viungo hivyo vitapatikana kwa gharama nafuu mara
utakapokamilika mradi huo.
Meghjee
aliongeza kuwa wakati wakiendesha ujenzi wa jengo la mapumziko katika Hospitali
ya Sekou Toure,walipata wazo la kujenga mabanda yatakayotumiwa na madereva wa
pikipiki (boda boda) kuegesha vyombo vyao kivulini na kupata huduma ya vyoo na
mabafu.
Mwenyekiti
huyo wa TD & CF aliongeza zaidi kuwa endapo Halmashauri ya Jiji itaridhia
na kuwapa eneo maalumu na mahususi la ujenzi wa huduma hiyo watafanya jaribio
hilo moja ili kuweza kuona matunda yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “VYOO 100 KUJENGWA BARABARA YA MWANZA KWENDA DAR ES SALAAM”
Post a Comment