Wednesday, November 16, 2016
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
Do you like this story?
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya
misako, Operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti
uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine
katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio
makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana
na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na wahalifu. Jitihada zinaendelea kwa
kushirikiana na wananchi kuhakikisha Mkoa wetu unakuwa mahala salama. Hata
hivyo kumekuwa na tukio 01 la mauaji kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 15.12.2016 majira ya saa 03:00 usiku
huko katika maeneo ya Mlima Reli, Kata ya Utengule – Usongwe, Tarafa ya Bonde
la Usongwe, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya, Mtu mmoja aliyetambulika
kwa jina la ISAMBI YELA (36) Mkazi wa Mwashiwawala alikutwa ameuawa kwa kukatwa
kichwa na miguu na mtu/watu wasiofahamika.
Chanzo cha mauaji hayo inadaiwa kuwa ni tuhuma za
wizi baada ya marehemu kukutwa amevunja nyumba mali ya PETER EDWIN (40) Mkazi
wa Mlima Reli Mbalizi kwa nia ya kuiba.
Aidha katika tukio hilo, mwili wa marehemu ulikutwa
hauna ubongo, baadhi ya meno yakiwa yameng’olewa, jicho la kushoto limetolewa
na mguu wa kulia ukiwa umekatwa na kuvunjwa.
Mtuhumiwa mmoja amekamatwa kwa mahojiano kuhusiana
na tukio hili ambaye ni PETER EDWIN ambaye nae alikutwa na majeraha sehemu ya
mdomoni. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Ifisi kwa
uchunguzi zaidi wa kitabib.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa
Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa kwa yeyote mwenye taarifa za mtu/watu
waliohusika katika tukio la kikatili kutoa taarifa ya siri kwa Jeshi la Polisi
ili kufanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao. Aidha anatoa wito kwa wananchi
kuacha kutafuta mali kwa njia ya mkato na badala yake wafanye kazi halali kwa
ajili ya kujipatia kipato na sio kujihusisha na uhalifu.
Imesainiwa na:
[DHAHIRI A. KIDAVASHARI – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA”
Post a Comment