|
Wakuu wa Wilaya wapya wa Mkoa wa Mbeya.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
|
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bw William Ntinika akiapa Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Mkalla.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
|
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mh Chalya Nyangindu akiapa Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Mkalla.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
|
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh Undalusyege Kitta akiapa Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Mkalla.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
|
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mh Reuben Mfune akiapa Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Mkalla.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
|
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh Rehema Madusa akiapa Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Mkalla.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewataka wakuu wapya wa wilaya kuifanya siku ya
alhamis ya kila wiki kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa
haraka na muhutasari huo umfikie mezani kila Jtatu ya kila wiki.
Amesema baadhi ya wananchi wanachukia serikali kutokana na kutopatiwa majibu ya
changamoto zao na urasimu baadhi ya viongozi na watendaji hivyo ni vema siku hiyo moja katika wiki ikawa siku ya wazi kwa
ajili ya kusikiliza kero za wananchi tu kama ambavyo yeye Mkuu wa Mkoa
alivyotenga siku ya Alhamis ya mwanzo wa mwezi na Alhamis ya mwisho wa mwezi ni
kwa ajili ya kusikiliza Kero za wananchi.
Amewataka kupitia kamati za ulinzi na usalama
wadumishe amani na utulivu na kudhibiti vitendo vya uhalifu na ujambazi wa
kutumia silaha
Aidha amewaagiza kufuatilia na kuhamasisha shughuli
za maendeleo na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha kwa miradi inayotekelezwa
katika halmashauri zao.
0 Responses to “MKUU WA MKOA WA MBEYA AMOSI MAKALA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WAPYA.”
Post a Comment