Thursday, July 21, 2016
NCCR WAMTIMUA MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA
Do you like this story?
Chama cha
NCCR – Mageuzi kimemvua uanachama makamu mwenyekiti wake (Bara), Leticia Ghati
(pichani) kikimtuhumu kujihusisha na migogoro ndani ya chama na tuhuma nyingine
za kijinai.
Mwenyekiti
wa chama hicho, James Mbatia aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa uamuzi
huo umepitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.
Mbunge
huyo wa Vunjo na mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alisema makosa mengine aliyokutwa
nayo Ghati ni pamoja na kukashifu na kutoa tuhuma dhidi ya kiongozi wa chama
nje ya utaratibu na kuhujumu chama wakati wa uchaguzi.
“Kwa
makosa hayo ambayo Leticia Ghati aliyatenda wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015
Halmashauri Kuu ya Taifa, inamsimamisha uongozi na kumvua uanachama,” alisema Mbatia.
Mustakabali
wa chama
Akizungumzia mustakabali wa chama hicho katika Ukawa, Mbatia alisema Halmashauri Kuu ya chama hicho itaendelea kusimama imara kuhakikisha umoja huo unakuwa bora na taifa linapata Katiba kama yalivyokuwa malengo ya kuanzishwa kwake.
Akizungumzia mustakabali wa chama hicho katika Ukawa, Mbatia alisema Halmashauri Kuu ya chama hicho itaendelea kusimama imara kuhakikisha umoja huo unakuwa bora na taifa linapata Katiba kama yalivyokuwa malengo ya kuanzishwa kwake.
“NCCR
tutahakikisha Ukawa unaboreka na kusimama imara kwa ajili ya kupata Katiba,
tumeazimia kuunga mkono jitihada za kuunganisha vyama vinavyounda umoja huu ili
kufikia lengo la kuwa na chama kimoja cha siasa chenye nguvu,” alisema Mbatia.
Mbatia pia
alizungumzia hali ya kisiasa na kidemokrasia nchini na kusema chama chake
kimebaini kuwa taifa linaongozwa kwa matamko ya Rais John Magufuli badala ya
kufuata Katiba, sheria na kanuni.
Alisema
demokrasia imeendelea kukiukwa huku uhuru wa kujieleza ukiendelea kudidimizwa
na akatolea mfano mwenendo wa Bunge ambao alisema licha ya kuwa chombo cha
kikatiba chenye mamlaka kamili ya kujiendesha, limeanza kuingiliwa katika
uendeshaji wake kwa wabunge kunyimwa fursa ya kujadili kwa uwazi masuala ya
Watanzania.
Alisema
NCCR inakemea matu- mizi ya nguvu za dola kupitia Jeshi la Polisi kuzuia
mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kuwakamata na kuwaweka rumande viongozi
wa kisiasa na kuwashtaki kwa makosa mbalimbali.
“NCCR
Mageuzi tunalaani tabia ya polisi kuwakamata na kuwahoji mara kwa mara viongozi
wa kisiasa na kuwashtaki kwa makosa mbalimbali… vitendo hivi ni ukiukaji wa
uhuru na haki za vyama vya siasa katika kufanya kazi zao,” alisema Mbatia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NCCR WAMTIMUA MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA”
Post a Comment