Thursday, July 21, 2016
VIGOGO OFISI YA WAZIRI MKUU KORTINI KWA WIZI
Do you like this story?
MAOFISA
Ugavi wanne wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kitengo cha Maafa), wamepandishwa
kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa madai
ya kuiba mali za ofisi hiyo zenye thamani ya Sh milioni 100.
Wakisomewa
hati ya mashtaka mbele ya Hakimu, Respicius Mwijage, Wakili wa Serikali,
Jackson Chidunda aliwataja washtakiwa hao, kuwa ni Ahmed Yusuph(48) Ofisa
ugavi, Martine Tyeah(31) Ofisa Ugavi Msaidizi, Mwahija Kimata(55),Ofisa ugavi
msaidizi na Halima Mwanjiro(33) Ofisa Ugavi.
Alidai
washtakiwa hao, wanadaiwa kati ya Aprili, 2014 na Septemba, mwaka huo huo
katika eneo la Keko lililopo karibu na Ofisi ya Bohari Kuu ya Madawa(MSD),
Temeke jijini Dar es Salaam, wakiwa waajiriwa wa Ofisi ya Waziri Mkuu,
wanadaiwa kuiba mabati 5074,Sufuria 200 na mikeka 348 vyenye thamani ya
Sh 100,164,000.
Alidai
mali hizo zinamilikiwana Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa ambazo
zilitolewa kwa ajili ya maafa kupitia kitengo hicho, lakini washtakiwa hao
wanadaiwa kuchukua kinyume cha sheria.
Alidai
upelelezi wa shauri hilo,bado haujakamilika na kuiomba mahakama hiyo kupanga
tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hata
hivyo, Hakimu Mwijage aliwataka kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja ambaye
atasaini bondi ya Sh milioni 25 ambapo washtakiwa hao walikidhi mashart hayo na
kuachiliwa kwa dhamana.
Shauri
hilo, limeahirishwa hadi Agosti 22, litakapotajwa tena.
Wakati huo
huo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempandisha kizimbani raia wa China,
Senxin Van baada ya kubainika kufanya kazi kinyume na kibali chake.
Akisomewa
hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Huruma Shahidi, Wakili wa Serikali, Novatus
Mlay alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Julai, 12, mwaka huu katika
kampuni ya uwekezaji ya Tenglong iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo
aliajiriwa kama daktari wakati kibali chake kinamruhusu kufanya kazi katika
kampuni ya kutengeneza viatu ya Tong Xing kama Mkurugenzi.
Katika
utetezi wake, mshtakiwa huyo aliiomba mahakama hiyo kumsamehe kwa sababu ni
babu mwenye wajukuu na mlezi wa familia na kwamba katika kampuni hiyo ni
Mkurugenzi ambaye ameajiri watanzania wengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “VIGOGO OFISI YA WAZIRI MKUU KORTINI KWA WIZI”
Post a Comment