Thursday, July 21, 2016
URUSI YAJIONDOA KWENYE MASHINDANO YA OLIMPIKI
Do you like this story?
SERIKALI ya Urusi imetoa tamko leo kuwa, wanariadha
wake hawatashiriki michezo ya Olimpiki ya mwaka huu huko Rio De Jenairo,
Brazil.
Kauli
hiyo imeafikiwa na mahakama ya juu ya michezo ambayo imefutilia mbali rufaa
iliyowasilishwa na kamati ya olimpiki ya Urusi ROC ya kuitaka ibatilishe uamuzi
wa shirikisho la riadha duniani IAAF wa kuwapiga marufuku wanariadha wake wote
wasishiriki michezo ya olimpiki itakayoandaliwa jijini Rio De Jenairo Brazil
kuanzia mwezi ujao.
IAAF
ilifikia uamuzi huo baada ya kugundua kuwa serikali ya Urusi ilikuwa na mpango
wa chini kwa chini wa kuficha matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku miongoni
mwa wanariadha wake.
Kamati
ya olimpiki ya Urusi ilikuwa imekata rufaa kwa pamoja na takriban wanariadha 68
ambao hawajawahi kupatikana na hatia ya matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku
ya kuongeza nguvu mwilini.
Baada
ya kusikiza pande zote mbili mahakama hiyo ya juu katika riadha CAS imeamua
kufutilia mbali rufaa hiyo.
Kauli
hiyo imewadia siku moja tu baada ya uchunguzi huru kubaini kuwa wizara ya
michezo ya Urusi, na kamati ya kupambana na matumizi ya madawa ya kuongeza
nguvu mwilini ya Urusi zilishiriki udanganyifu ikiwemo kubadilisha mikojo ya
wanariadha ilivipimo visipatikane na madawa hayo yaliyopigwa marufuku.
Kamati
ya Olimpiki ya Kimataifa IOC imesema itatathmini kwanza hatua za kisheria,
kabla ya kufanya uamuzi wowote kuhusu iwapo itaipiga marufuku Urusi kutoka
kwenye mashindano ya Olimpiki huko Rio de Janeiro Brazil.
Hatua
hii inafuatia ripoti huru kuhusu serikali kuhusika na kuwasaidia wanamichezo
wake katika matumizi ya madawa ya kusisimua misuli.
IOC
hata hivyo imewafungia maafisa wote wa Urusi kushiriki michuano ya Olimpiki ya
Rio, na itawapima tena wanamichezo walioshiriki michuano ya Olimpiki ya majira
ya baridi yaliyofanyika Sochi.
Tayari
wanariadha wa Urusi wamepigwa marufuku na IAAF.
Shirikisho
la riadha IAAF limefurahia kauli hiyo ya mahakama ya juu ya michezo ikisema
kuwa imesawazisha uwanja wa riadha.
”Kwa
hakika tumefurahi kuwa CAS imeunga mkono kauli yetu. Leo kwa hakika sio siku ya
kufurahia kwani IAAF haikuja katika michezo kuwazuia wanariadha wasishiriki
katika michezo ila nia yetu ni kusawazisha uwanja ili
wanariadha
wote washindane kw mizani sawa” alisema rais wa shirikisho la riadha Lord
Sebastian Coe.
”Baada
ya rio tutaendelea kuisaidia kamati ya olimpiki ya urusi ilikuwaruhusu
wanariadha wake kurejea katika mashindano ya kimataifa.” aliongezea Coe.
Licha
ya uamuzi huo wa CAS,wanariadha wachache wa urusi ambao watakubali kushiriki
chini ya bendera ya kamati ya olimpiki wataruhusiwa kushiriki ila lazima
wapitie vipimo za ziada ilikuthibitisha kuwa ni wasafi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ URUSI YAJIONDOA KWENYE MASHINDANO YA OLIMPIKI”
Post a Comment