Friday, July 22, 2016
HUKUMU KUMHUSU ANAYEDAIWA KUMUUA DAUDI MWANGOSI
Do you like this story?
HUKUMU ya kesi ya mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi iliyokuwa itolewe
leo, Julai 21, 2016 imeahirishwa hadi Jumatatu Julai 25.
Kesi hiyo inayomkabili askari Polisi Pacificius Cleophace Simoni ambaye
hivi karibuni alijitetea kwa kupinga kuhusika na mauaji hayo.
Akiahirisha
hukumu ya kesi hiyo, Kaimu Msajili wa Mahakama hiyo, Jofrey Isaya alisema
inaahirishwa kwasababu Jaji Paulo Kiwehlo aliyekuwa akiisikiliza yuko nje ya
Iringa kwa majukumu mengine ya kikazi.
Kabla ya
kuanza kwa shughuli za kimahakama, hofu ilitanda kwa wanahabari na watu wengine
waliojitokeza kwa wingi kusikiliza hukumu hiyo kutokana na idadi kubwa ya
askari Polisi, wenye sare na wasio na sare, waliokuwepo nje na ndani ya viunga
vya mahakama hiyo.
Katika hali
isiyo ya kawaida, kila aliyekuwa akiingia ndani ya viunga vya mahakama hiyo kwa
kupitia lango kuu alikuwa akigaguliwa na Polisi hao walioondoka mara tu baada
ya hukumu ya kesi hiyo kuahirishwa.
Pamoja na
askari hao kulikuwepo na magari ya Polisi, yakiwemo mawili aina ya Landlover
Defender ambayo mojawapo hutumika kumleta mtuhumiwa huyo tofauti na gari
linalotumiwa kuwaleta watuhumiwa wengine wa kesi mbalimbali mahakamani hapo.
Chumba cha
mahakama kilichotumika kuahirisha kesi hiyo kilikuwa na askari zaidi ya 20,
wakiwemo waliobeba silaha kali za moto hali iliyokuwa ikitishia utendaji kazi
wa baadhi ya wanahabari ambao mara kwa mara wamekuwa wakizuiwa na askari hao
kupiga picha kabla ya kuanza kwa shughuli ya mahakama.
Rais wa
Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deo Nsokolo aliunga na
wanahabari zaidi ya 20 wa mjini Iringa na kushuhudia jinsi wanahabari
wanavyopata misukusuko wakati wa kuripoti kesi hiyo.
“Nimekuja
mjini Iringa kuuungana na wanahabari wa mkoa wa Iringa na kuwawakilisha
wanahari nchini kote kusikiliza hukumu ya kesi hii ambayo ni muhimu sana kwa
tasnia ya habari hapa nchini,” alisema.
Kaimu
Msemaji wa Mahakama hiyo, Lusako Mwang’onda alisema mahakama hiyo itahakikisha
wanahabari wanapata haki yao ya kimsingi ya kupata habari wawapo mahakamani.
Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba hakuweza kupatikana ili atoe ufafanuzi
wa yale yanayojitokeza mahakamani kila mtuhumiwa huyo anapofikishwa mahakamani
hapo.
Kwa mara ya kwanza Simoni alifikishwa mahakamani hapo Septemba 12, 2012
akituhumiwa kumuua Mwangosi kwa kukusudia katika tukio lilitokea katika kijiji
cha Nyololo, wilayani Mufindi Mkoani Iringa Septemba 2, 2012 wakati mwandishi
huyo alipokuwa akiwajibika katika kazi zake za kutafuta habari wakati wa ufunguzi
wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
chanzo ni bongo leak blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ HUKUMU KUMHUSU ANAYEDAIWA KUMUUA DAUDI MWANGOSI”
Post a Comment