Friday, July 22, 2016
KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM MJINI DODOMA LEO..... AMPA TAHADHALI RAIS MAGUFULI
Do you like this story?
JAKAYA
Kikwete, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) anayemaliza muda wake
amemtahadharisha mwenyekiti mtarajiwa wa Chama hicho John Magufuli kwa
kumweleza kuwa uenyekiti ndani ya CCM siyo lelemama kwani wajumbe wasipoelewa
wanachokitaka.
Mbali na kumpa tahadhari hiyo pia alikiri kuwa mwaka jana chama hicho kilikumbwa na misukosuko mingi ambayo ingeweza kukifanya chama hicho kuanguka kwani kilikuwa na mafisi wengi ambao walikuwa wakisubiri mkono udondoke ili washibe
Ametoa
kauli hiyo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho
ambayo ajenda ilikuwa moja tu ya kujadili na kupitisha jina la mwenyekiti
ambalo litapelekwa katika mkutano mkuu kwa lengo la kupigiwa kura.
Kikwete
amesema ..."CCM ilikuwa ivunjike wakati wa kipindi kigumu cha uchaguzi
wa mwaka jana lakini tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumeweza kukaa imara na
kukitafa chama kutovunjika.
“Tunasema
kikao kama hiki hatumwi mtoto tunakuja wenyewe kikao cha leo ni kikao cha
kihistoria, kwa mamna mbili kwanza ni kikao changu cha mwisho, nikija kwenye
NEC ni pale mtakapo nialika lakini tulikubaliana kwamba wazee hao
wameishatumikia vya kutosha na tuwaache wapumzike utaratibu wa hapo nyuma
ukimaliza uenyekiti unakuwa mjumbe wa kudumu wa kamati kuu na halmashauri kuu.
“Siku
moja Mzee Mkapa akasema bwana mbona sisi wazee mnatusumbua sana mnatuita kila
siku na sisi tumeishakuwa wazee tunakaa mpaka saa saba usiku kwa hivi sasa
tuacheni, ndipo niliposema hatuwezi na tukaamua kuunda baraza la wazee.
“Tukaona
hatuwezi kuwaita kila siku lakini tunawatengenezea baraza la wazee ambalo ni
baraza la ushauri kimsingi linahitajika kwa jambo muhimu sana kama ilivyo kuwa
mwaka lakini nilijadiliwa nikaambiwa JK hataki wazee lakini nikasema huo ni
uamuzi wa busara kabisa” amesema Kikwete.
“Kuna
maswala makubwa ya chama chetu na uhai wake kama ilivyokuwa mwaka wa jana, eeee
chama chetu kilikuwa kimekaa katika msukosuko mkubwa mnaingia hapa watu
wanaimba hiki wanaimba kile mjadala mkali lakini nikasema tutavuka tu maadamu
tupo ndiyo changamoto ya uongozi.
“Na
maadamu CCM haikuvunjika mwaka wa jana haitavunjika tena, maana mafisi yalikaa
hapa yanasubiri mkono udondoke lakini haukudondoka na maadam haukudondoka mwaka
wa jana CCM haidondoki,”amesema
Kikwete.
Amesema
rais atakuwa mwenyekiti na wakati mwingine kuna wakati kikao kinakuwa kigumu
kwani wajumbe wanataka kutendewa haki wa wasipopata haki zao wanakuwa wakali
sana.
Amesema
halmashauri kuu ni kikao Muhimu cha uongozi pale ambapo hakuna mikutano ya
chama amesema kamati kuu ni kikao cha kusimamia shughuli muhimu za chama na NEC
ni kikao cha juu cha kutoa viongozi.
Amesema
wajumbe wa vikao ni wepesi sana kusifia lakini wanakuwa wakali sana pale ambapo
mambo yanaenda vibaya hivyo kiongozi ni lazima kumsikiliza na kujua nini
ambacho wajumbe wanataka.
Amesema
wajumbe hao wanakuwa wakali kwa kuwa wanataka mambo ndani ya chama yaende
vizuri ili nao ndani ya chama waweze kujivunia.
Mbali na
hayo amesema wajumbe wanatakiwa kushirikiana na mwenyekiti mpya ili kukifanya
chama kuweza kusonga mbele zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM MJINI DODOMA LEO..... AMPA TAHADHALI RAIS MAGUFULI”
Post a Comment