Friday, July 22, 2016
KESI YA UHUJUMU UCHUMI ZAIGIZA BILIONI 29.
Do you like this story?
Waziri wa
Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema Mahakama Kuu chini ya kitengo
kinachosimamia kesi za kuhujumu uchumi imetoa adhabu ya kifungo na kulipa faini
ya Sh29 bilioni kwa watu 12 baada ya kutiwa hatiani.
Pia,
alisema Mahakama ya Mafisadi iliyoahidiwa na Rais John Magufuli wakati wa
Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, itakapoanza itashugulikia kesi za ufisadi zenye
ushahidi.
Dk
Mwakyembe alisema hayo jana kwenye mahojiano katika kipindi cha 360 kinachorushwa
moja kwa moja, asubuhi siku za wiki na Televisheni ya Clouds.
“Tuna
kesi 176 za kuhujumu uchumi tangu Juni mwaka jana hadi sasa. Kesi 13
zimekamilika, watu 12 wamehukumiwa vifungo vya jela na tunawadai Sh29 bilioni
kwa hiyo kama mtu alikuwa na ‘kastore’ tutauza tupate hiyo pesa,” alisema Dk Mwakyembe.
Aliongeza:
“Nchi ilipofikia tunataka tuachane na hizi tabia za udokozi unapopewa
mamlaka ya kuhudumia umma.”
Alipoulizwa
kuhusu mahakama ya mafisadi alisema: “Hatujaanzisha Mahakama, tumeanzisha
divisheni (kitengo) ambacho kitasimamia kesi hizo kwa haraka na kwa weledi
zaidi.”
Itakumbukwa
kuwa Aprili Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasilisha hotuba ya
makadirio na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni alisema Serikali imeanzisha
Divisheni ya Rushwa na Ufisadi ya Mahakama Kuu.
Majaliwa
alisema mahakama hiyo itaanza kushughulikia kesi 10. Dk Mwakyembe alipoulizwa
kama kuna kesi zozote zinazohusu EPA, Escrow au Richmond zitakazo sikilizwa,
alijibu: “Sheria tunayotumia ni kwamba, kesi za jinai hazina vizuizi kwa
upande wa Jamhuri.Hata kama ulichukuwa miaka 20 iliyopita, kama ushahidi
unapatikana tutaendelea. Lakini hatuna interest kufufua makaburi ya huko
nyuma.”
Kuhusu
mchakato wa Katiba inayopendekezwa alisema: “Ni kiporo ambacho tumepokea
Serikali ya awamu ya tano na lazima tukimalize.”
Alisema
kinachofanyika sasa ni kufuata Katiba kwa sababu mchakato huo ulisimama kupisha
Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
“Tusingeweza
kusimamisha uchaguzi kwa ajili ya kupiga kura ya maoni. Kwa hiyo tunasubiri
wenzetu NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) wawe tayari ili mchakato uweze
kuendelea,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ KESI YA UHUJUMU UCHUMI ZAIGIZA BILIONI 29.”
Post a Comment