Saturday, July 23, 2016
VIGOGO WOTE WAKALA WA MISITU TANZANIA (TFS)WATUMBULIWA MAJIPU.
Do you like this story?
SERIKALI
imemuondoa katika nafasi yake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS),
Gerald Kamwenda na wakurugenzi wenzake, katika jitihada za kufumua na kusuka
upya shirika hilo.
Waziri wa
Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, ametangaza hatua hiyo ya
serikali jana alipokutana na vyombo vya habari na kuongeza kuwa, watumishi
wengine 41 wamehamishwa vituo vya kazi.
Alifafanua
kuwa hatua hizo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa, lililotaka kufumuliwa na kusukwa upya kwa TFS ili kuongeza ufanisi.
Kutokana
na hatua hiyo, Waziri Maghembe alisema Profesa Dos Santos Silayo ameteuliwa
kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TFS, wakati Kamwenda anahamishiwa Chuo cha Viwanda
vya Misitu kilichopo Moshi.
Aidha,
Mwanaidi Kijazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Raslimali za Misitu na
Nyuki, yeye amekwenda kuwa Mhifadhi Mkuu Amani Nature Reserve na nafasi yake
inachukuliwa na Zawadi Mbwambo.
Waziri
Maghembe alisema Mohamed Kilongo aliyesimamishwa kazi Januari 5, mwaka huu
uchunguzi umeonekana hana hatia na hivyo anaendelea kuwa Mkurugenzi Mipango na
Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu.
Alisema
Wizara imeamua Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Gladnes Mkamba
ahamishiwe Idara ya Mipango makao makuu na nafasi hiyo kuteuliwa Dk Ezekiel
Mwakalukwa, kuwa Kaimu Mkurugenzi.
Aidha
Monica Kagya aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki,
anakuwa Mtafiti Mwandamizi Idara ya Nyuki (Tawiri). Alisema Kagya ni mtaalamu
wa masuala ya nyuki, hivyo atahamishiwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori, ili
ashughulikie utafiti wa masuala ya nyuki.
Pia
alisema katika Idara ya Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa anakuwa Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na
Herman Kerayo ambaye anahamishiwa Idara ya Mipango Makao Makuu.
Profesa
Ramadhan Kideghesho, yeye anakwenda kuwa Mkuu wa Chuo cha Mweka wakati Mabula
Misungwi aliyekuwa Meneja Mradi Selous, anakwenda Chuo cha Wanyamapori Pasiansi
na nafasi yake inachukuliwa na Jaffary Lyimo, huku Robert Mande akipelekwa kuwa
Kaimu Mkurugenzi msaidizi Uzuiaji Ujangili.
Waziri
Maghembe alisema Majjid Ally ameteuliwa kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Leseni,
nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Haji Mpya ambaye amehamishiwa Shamba Jipya
Songea kuwa Ofisa Misitu Alisema Julai 18, mwaka huu Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa alikutana na viongozi na watumishi wa Wizara hiyo na watendaji wakuu
na watumishi wa TFS na kuagiza kufumuliwa na kusukwa upya kwa wakala huo.
Katika
mkutano huo, Waziri Mkuu alitaka kuondolewa kwa utitiri wa vituo vya ukaguzi na
kuwekwa vituo vichache na kuondolewa kwa ofisi za makontena yanayotumiwa na
ofisi ya TFS, badala yake watumishi wanaofanya ukaguzi wasimame maha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “VIGOGO WOTE WAKALA WA MISITU TANZANIA (TFS)WATUMBULIWA MAJIPU.”
Post a Comment