Saturday, July 23, 2016

RAIS MAGUFULI AVUNJA REKODI YA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA CCM TAIFA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amevunja rekodi baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kwa kupata asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa.

Rekodi hiyo ya kupata asilimia 100  ya kura zote kwenye uchaguzi wa aina hiyo (Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa) haijawahi kufikiwa na kiongozi yeyote ndani ya CCM tangu kuanzishwa kwa chama hico Februari 5, 1977 ambapo ni miaka 39 sasa.

Wenyeviti wa CCM waliyopita ambao ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa wala Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete hawakuwahi kupata kura zote zilizopigwa kwenye uchaguzi wa ngazi hiyo.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliyofanyika mjini Dodoma leo, Mwenyekiti wa CCM aliyemaliza muda wake, Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema matokeo kuwa; ifuatavyo
Kura zilizopigwa zilikuwa ni 2398, kura halali ni 2398, kura zilizoharibika ni 0, kura za hapana ni 0 na kura za Ndiyo ni 2398.

Baada ya kumtangaza mshindi, Dkt. Kikwete alimkabidhi Mwenyekiti mpya Dkt. Magufuli nyaraka za uongozi na baada ya hapo Dkt. Kikwete alitangaza kustaafu rasmi Uenyekiti wa CCM na kumuachia Dkt. Magufuli aongoze kwa miaka mitano ijayo.

0 Responses to “RAIS MAGUFULI AVUNJA REKODI YA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA CCM TAIFA”

Post a Comment

More to Read