Tuesday, July 12, 2016
SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU UHABU WA MAFUTA YA PETROL NA TAA HAPA NCHINI
Do you like this story?
MAMLAKA ya
Udhibiti ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuna akiba ya kutosha ya
mafuta ya aina mbalimbali yanayoweza kutumika kati siku 13 hadi 39 nchini.
Mkurugenzi
Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana katika
mkutano na wadau wa sekta ya mafuta nchini wa kupokea maoni juu ya mfumo wa
uingizaji wa mafuta nchini.
Tamko la
EWURA limekuja kukiwa na tatizo la uhaba wa mafuta ya petrol, dizeli na mafuta
ya taa katika baadhi ya mikoa hali iliyosababisha wananchi wa mikoa iliyokumbwa
na tatizo hilo kupata adha.
Ngalamgosi
alisema akiba ya mafuta ya ndege iliyopo inatosha kutumika kwa siku 30 kwa
nchini nzima, petroli ni zaidi ya siku 12, dizeli ni zaidi ya siku 15, mafuta
ya taa ni zaidi ya siku 16, mafuta ya viwandani ni zaidi ya siku 39 na mafuta
ya migodini zaidi ya siku 13.
Alisema
sababu ya kutokea uhaba wa mafuta unaoonekana sasa ni kuwepo kwa sikukuu
zilizofululiza na kusababisha magari ya kubeba mafuta kushindwa kusafirisha
mafuta, na ama kufika kwa wakati katika mikoa hiyo iliyokubwa na kadhia hiyo.
Jumatano
na Alhamisi zilizopita palikuwa na siku kuu za Eid el Fitri.
“Niwaombe
Watanzania wawe na subira kwani mafuta yapo yakutosha, hivyo nawaomba wasinunue
mafuta kwa kupaniki kwani magari ya kusafirisha mafuta yameanza kusambaza
katika mikoa hiyo na hali itatulia kuanzia sasa,” alisema.
Alisema
magari ya mafuta yameshapeleka shehena katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Songea
na Mbinga ambako hali ya upatikanaji wa mafuta imeanza kutulia.
Mafuta
ya taa
Ngalamgosi
alisema uhaba wa mafuta ya taa ulitokana na meli iliyokuwa ikishusha mafuta ya
ndege na petroli kuyachaganya wakati wa kuyasukuma.
Alisema
kuwa kutokana na mchanganyiko huo ni wazi kuwa mafuta ya ndege ambayo ndio
hutumika kama mafuta ya taa, hayaweza kutumika kwa matumizi ya kawaida.
“Mafuta
ya ndege ndio hayo hayo yanatumika kama mafuta ya taa hivyo kutokana na
kuchanganyika huko ilipaswa kusafisha matanki yote na mabomba ili kuweka mafuta
mapya,” alisema.
Alisema
zoezi la kuyasafisha matanki matano lilifanyika kwa wiki tatu mfululizo na
kukamilika Julai 2, kabla ya kuanza kupokea mafuta na kuyasambaza Julai 3 mwaka
huu katika mikoa ambayo kulitokea uhaba.
Kampuni
za ndani
Ngalamgosi
alisema EWURA imependekeza kubadilishwa kwa mfumo wa uingizwaji wa mafuta
nchini kutoka nchini za nje kwa kuanzishwa mfumo mpya wa kutoa fursa kwa
kampuni za ndani kuingiza mafuta nchini.
Ngalamgosi
alisema kuwa amekutana na wadau wa sekta ya mafuta ili kupokea maoni ni namna
gani wanaweza kuboresha ushindani na wamependekeza kuwa kila meli inayokuja
lazima iwe na zabuni yake.
Alisema
Tanzania inaingiza meli sita za mafuta kwa mwezi, hivyo EWURA imeona kuwa
inapasa kuwa kila meli ya mafuta inayoingia iwe zabuni inayojitegemea.
“Kwa
kufanya hivyo kutatoa fursa kwa watanzania kuweza kuingiza mafuta kwa sababu
itapunguza gharama na uzuri utakuwa nchi itanufaika kuwa na watanzania wengi
kushiriki katika kuingiza mafuta,”alisema.
Aliongeza
kuwa kupita utaratibu mpya wanaamini kuwa makampuni ya Tanzania yatapata faida kubwa
na TRA kukusanya mapato mengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU UHABU WA MAFUTA YA PETROL NA TAA HAPA NCHINI”
Post a Comment