Thursday, July 28, 2016
SIKU YA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MAMIA WAJITOKEZA ,RC AWATAKA WATENDAJI SERIKALINI KUWA KARIBU NA WANANCHI.
Do you like this story?
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw Amosi Makalla akifungua kikao cha wananchi kueleza kero zao.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Baadhi wa wananchi waliotoka sehemu Mbalimbali za Mkoa wa Mbeya wakisubili kutoa kero zao kwa Mkuu wa Mkoa |
Baadhi ya watendaji wa Serikali wakiwa wanasikiliza kero za wananchi Mbalimbali waliofika leo kwaajili ya kutoa kero zao(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Wafanyabiashara Ndogondogo pia wakitoa kero zao za Muda Mrefu ambazo hazijafanyiwa kazi hadi sasa. |
Mzee akitoa Kero zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla leo ameendelea na utaratibu aliyojiwekea wa
kusikiliza Kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi
kila siku ya Alhamisi ya mwanzo wa mwezi na siku ya alhamis ya mwisho wa mwezi
kama kawaida siku ya leo mamia ya wananchi wamejitokeza Mbele ya Mkuu wa Mkoa
kuwasilisha kero zao.
Mkuu wa Mkoa amewataka wakuu wa wilaya na watendaji wa ngazi zote kuwasikiliza wananchi na kutatua Kero zao
" Kero Nyingi hapa ni za
halmashauri, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wakuu wa idara tafadhalini hakuna
jambo kubwa katika uongozi kama kuwa Karibu na unaowaongoza, kuwa msikivu na
kushughulikia matatizo yao kwa umati huu ni dhahiri hamjatimiza majukumu yenu
na kwa kuwa MaDc, ma Ded ni wapya sasa anzeni kazi hii kwa kasi "
Amekitaka jeshi la polisi kuharakisha upelelezi wa kesi na pia kuepuka vitendo vinavyolalamikiwa kwa baadhi ya askari kubambikizia wananchi kesi.
Amehaidi kuendeleza utaratibu huu kwa muda wote mpaka siku atakapofika ukumbini akute hakuna Mwananchi aliyeleta Kero
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIKU YA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MAMIA WAJITOKEZA ,RC AWATAKA WATENDAJI SERIKALINI KUWA KARIBU NA WANANCHI.”
Post a Comment