Thursday, July 28, 2016
MWIGULU NCHEMBA ATUA MGODI WA NYAMHUNA UNAODAIWA KUTESA NA KUUA MTANZANIA MMOJA, AWAKAMATA WAHUSIKA (WACHINA NA WATANZANIA) WANAOSADIKIKA KUHUSIKA.
Do you like this story?
Waziri wa mambo ya ndani ya
nchi Mwigulu Nchemba hii leo amewasili mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi kubwa
ikiwa ni kufuatia taarifa za mateso na mauaji yaliyofanywa na raia wa china
wanaomiliki sehemu ya mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro-Geita dhidi ya wafanyakazi/vibarua
ambao ni watanzania.
Takribani wiki moja sasa kumekuwa
hali ya sintofahamu dhidi ya picha zinazoenezwa mitandaoni na kwenye vyombo vya
habari zikionesha raia wa tanzania anayefanya kazi kwenye mgodi tajwa akiteswa
na kufanyiwa vitendo vya kinyama na mwajili wake ambaye ni raia wa china.
Imemlazimu waziri mwenye dhamana na
usalama wa raia na mali zao kupitia wizara ya mambo ya ndani kufika eneo la
mgodi kujiridhisha kwa taarifa zilizotapakaa na kubeba simanzi kwa watanzania.
Mwigulu Nchemba amejiridhisha kuwa
kulikuwepo na tukio hilo la mtanzania kuteswa na huyo mwajili wake kipigo
kilichopelekea kupoteza fahamu na sio kifo.
Hatua za awali mwigulu alizozifanya
ni kwenda gereza la Geita mjini alikohifadhiwa kijana huyo kwa madai
ameshitakiwa na mwajili wake kwa kosa la wizi lililopelekea yeye kupigwa.
Katika mahojiano ya waziri Mwigulu
Nchemba na kijana huyo,Mwigulu alibaini kuwa kijana huyo aliyepo gerezani ndiye
mhanga wa tukio lile kwa uthibitisho wa makovu yaliyopo mwili mwake na mavazi
aliyovalia wakati anateswa na wakati yupo hapo gerezani.
Katika hali hiyo ilimlazimi
Mh.Mwigulu kwenda mgodini akiwa ameambatana na kijana huyo kwaajili ya kutambua
waliofanya vitendo hivyo vya kinyama.Katika oparesheni hiyo, kijana aliyeteswa na kujeruhiwa aliwabaini
watanzania 5 ambao ni walinzi wa eneo hilo na mchina mmoja walioshirikiana
kumpiga,kumtesa na kumjeruhi.
Kufuatia utambuzi huo na maelezo ya
wahusika,Nchemba akaagiza wahusika wakamatwe mara moja na ameondoka nao kwa
hatua zaidi za kisheria.
Katika hali nyingine ya
kusikitisha,Mwigulu amebaini uwepo wa wahamiaji haramu raia wa china katika
mgodi huo ambapo nyaraka za uhamiaji mkoa wa geita zinainesha raia 28 wenye
vibali ndio waliruhusiwa kukaa kwenye mgodi huo,lakini katika operasheni ya
kushitukiza aliyoifanya Mh.Mwigulu nchemba amebaini uwepo wa raia wa china
zaidi ya 50 wanaoishi katika mgodi huo kinyume na sheria.Hivyo amemuagiza mkuu
wa mkoa na timu yake ya uhamiaji kuhakikisha wote wasio na vibali wanakamatwa
na kuchukuliwa hatua za kisheria
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWIGULU NCHEMBA ATUA MGODI WA NYAMHUNA UNAODAIWA KUTESA NA KUUA MTANZANIA MMOJA, AWAKAMATA WAHUSIKA (WACHINA NA WATANZANIA) WANAOSADIKIKA KUHUSIKA.”
Post a Comment