Thursday, July 28, 2016
WANAOTENGENEZA VYETI BANDIA VYA SERIKALI WAPEWA MWEZI MMOJA KUJISALIMISHA
Do you like this story?
MPIGACHAPA
Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo, ametoa mwezi mmoja kwa watu
wanaojihusisha na utengenezaji wa vyeti bandia vya Serikali kujisalimisha kabla
hawajachukuliwa hatua za sheria.
Hivi
karibuni Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam liliwakamata watu
watatu ambao walikutwa na vyeti bandia vya kidato cha nne, vyeti vya uuguzi,
stika za Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), vyeti
vya kuzaliwa na vyuo vya ufundi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Chibogoyo alisema wanakusudia kuendesha msako nchi
nzima kuwabaini watu hao na kuwachukulia hatua za sheria.
“Baada
ya muda tuliotoa kuisha tutafuatilia mkoa hadi mkoa kuhakikisha tunadhibiti
nyaraka bandia,” alisema Chibogoyo.
Aliwataka
Watanzania kuacha kutumia vibaya bendera, nembo na wimbo wa taifa kwa
sababu ni vielelezo vya taifa.
Alisema
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na ile inayopendekezwa,
zote zinaelekeza kuhusu matumizi bora ya vielelezo vya taifa kama vile bendera,
nembo na wimbo wa taifa.
“Bendera
iheshimiwe, hairuhusiwi kupeperusha bendera iliyotoboka, kupauka au chafu.
Katika maeneo mengine unaweza kukuta bendera inapandishwa au kushushwa lakini watu
wamekaa chini na wengine wanaendelea na shughuli zao,” alisema Kibogoyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WANAOTENGENEZA VYETI BANDIA VYA SERIKALI WAPEWA MWEZI MMOJA KUJISALIMISHA”
Post a Comment