Thursday, July 28, 2016

IVO MAPUNDA ATAFUTA TIMU ATAKAYOICHEZEA HAPA NCHINI.MBEYA


Kipa Mkongwe aliyekuwa anaichezea Timu ya Azam Fc Ivo Mapunda akiwa anafanya mazoezi  na Timu ya Tanzania Prisons jijini Mbeya.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Kipa Mkongwe aliyekuwa anaichezea Timu ya Azam Fc Ivo Mapunda akiwa anafanya mazoezi  na Timu ya Tanzania Prisons jijini Mbeya.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Kipa Mkongwe aliyekuwa anaichezea Timu ya Azam Fc Ivo Mapunda akiwa na Mtoto wake wa kwanza mara baada ya kumaliza mazoezi.


KIPA mkongwe aliyekuwa akiichezea Azam FC, msimu uliopita Ivo Mapunda, amesema baada ya kufanya mazungumzo na klabu ya AFC Leopards inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kenya, kwa sasa anaangali timu nzuri ya nyumbani itakayompa nafasi ya kuendeleza kipaji chake.

Amesema, klabu hiyo ya Leopards, amefanya nayo mazungumzo na kwa sasa anasubili majibu, pindi ligi kuu inayoendelea nchini humo itakapomalizika, lakini wakati akiendelea kusubili ni vema akaangali timu nzuri itakayoweza kumpa nafasi ya kucheza.

Ivo, aliyasema hayo jana, baada ya kumaliza kufanya mazoezi kwenye uwanja wa michezo unaomilikiwa na timu ya Tanzania Prisons, uliopo ndani ya Jeshi la Magereza Mkoani Mbeya.

Alisema,anachokifanya sasa ni kujiweka fiti kimchezo na ndio sababu iliyomfanya kuweka kambi Mkoani Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya michezo mingine, kwani lengo lake ni kuonyesha kipaji kwamba bado anauwezo licha ya baadhi ya timu za nyumbani kumuona  mzee amepitwa na wakati.

Aidha, akiizungumzia timu ya Tanzania Prisons, Mapunda alisema licha ya kupata muda mchache wa kuishuhudia timu hiyo ikifanya mazoezi lakini ameonesha kufurahishwa na usajili uliofanywa na uongozi wa klabu hiyo kwani umeonekana kukidhi vigezo na kuzingatia mapungufu yaliyokuiwa yamejitokeza wakati wa msimu wa ligi kuu uliomalizika.

Hata hivyo, Mapunda alitumia nafasi hii kuwasihii wachezaji wenzake kucheza mpira kwa maslahi ya Taifa na maisha yao na kuachana na mpira wa matangazo na sifa.

0 Responses to “ IVO MAPUNDA ATAFUTA TIMU ATAKAYOICHEZEA HAPA NCHINI.MBEYA”

Post a Comment

More to Read