Thursday, July 28, 2016

JIANDAE KUWAONA INTERCLUBE SIKU YA SIMBA DAY


Ndg. Ryaganda (Mwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EAG Group ) na Rais wa Simba Evans Aveva wakionesha tangazo la Simba Day 


Leo Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva ameongea na waandishi wa habari na kuwafahamisha watanzania na Dunia nzima ni  klabu ipi ya kimataifa ambayo itacheza na klabu ya Simba kwenye sherehe za Simba Day. 

Akiongea mchana wa leo  alisema “Klabu ya kimtaifa ambayo itakuja kucheza nasi ni Interclube kutoka nchini Angola”
Kaatika mkutano na waandishi wa habari mwakilishi wa Mkurugenzi wa kampuni ya EAG Group Limited ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya masoko na biashara wa Simba Ndg. Richard Ryaganda, alitumia fursa hiyo kuweza kushukuru vyombo vya habari katika kuisaidia klabu ya Simba kutoa taarifa zake kwa watanzania na Duniani kwa ujumla.


Rais Wa Simba Evans Aveva



“ Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group Imani Kajula ambaye amepata dharura hivyo kupelekea leo kushindwa kufika hapa, tunapenda kuwashukuru sana kwa kuwa nasi siku zote katika kuhabarisha umma kuhusiana na mambo mbalimbali katika klabu yetu ya Simba hususani kwenye Simba Week na Simba Day” alisema Ndg. Ryaganda 

 




Hii ndio hutuba ya Rais wa klabu ya Simba:

HOTUBA YA RAIS WA SIMBA SPORTS CLUB EVANS AVEVA WAKATI WA KUZINDUA WIKI YA SIMBA NA SIMBA DAY 2016 .
Viongozi wenzangu wa Simba,
Mwakilishi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group Richard Ryaganda,
Waandishi wa habari,
Mabibi na mabwana,

Habari za asubuhi,
Napenda niwashukuru sana kwa kufika kwenu hapa, pia kwa namna ya kipekee niwashukuru kwa kuendelea kuwapa habari Watanzania kupitia vyombo vyenu.
Kama wengi mnavyojua kila mwezi Agosti, Simba inasherehekea wiki maalum iliyobatizwa jina la Simba Week ambayo hufikia kilele chake tarehe 8 Mwezi wa Agosti. Mwaka huu siku hii itakuwa na uzito wa kipekee kwani Klabu ya Simba itakuwa inaanza sherehe za kuadhimisha miaka 80 ya klabu yetu tukufu.
Sherehe za Wiki ya Simba zinaenda sambamba na dhima yetu ya kuendeleza mabadiliko chanya ndani ya Simba bado inaendelea kushika kasi, Katika kipindi cha mwaka mzima, mmekuwa mashuhuda wa Simba inayolenga kuleta mapinduzi makubwa katika jinsi mpira unavyoendeshwa, kujali wanachama, utoaji wa taarifa kwa wapenzi na wanachama wake na kukuza vyanzo vya mapato na kuangalia njia zenye kuweza kuongeza ufanisi na maendeleo ya timu yetu ya Simba.

Ndugu wanahabari,
Kama nilivyoeleza awali , Simba imekuwa na utaratibu wa kuwa na siku maalum kwa ajili ya kufurahi, kuwatambulisha rasmi wachezaji, jezi za timu na kujiandaa kwa msimu mpya, siku huu imekuwa maarufu kama Simba Day. Tangu ianzishwe imekua ikiboreka siku hadi siku, mwaka huu tumeona ni muhimu kuiboresha zaidi na hususani kuangalia mchango wa timu yetu kwa jamii inayoizunguka.
Kuanzia mwaka jana Simba iliamua kuanzisha Simba Week ambayo lengo lake kuu ni kuwa wiki ya Simba Sports Club kufanya kazi za jamii, kukuza vipaji vya soka vya vijana, kutembelea wadau wa maendeleo na pia shughuli nyingine zenye tija kwa timu yetu na jamii kwa ujumla. Wiki hii itahitimishwa siku ya Simba Day ambapo mambo mengi mazuri yatafanyika. Kama ilivyokuwa mwaka jana, tutatengeneza program ambayo itawashirikisha wana Simba Nchi nzima. Tunategemea kuwa katika siku za kujitolea kwa jamii, wapenzi wote wa Simba Nchi nzima watajitokeza kufanya shughuli za kijamii kwenye maeneo yao. Simba inaamini kwa dhati tukiunganisha Nguvu zetu tunaweza kuleta madabiliko makubwa sana Nchini kwetu.
Ndugu wana habari,
Habari njema leo ni nyingi na ubunifu ni jadi yetu. Napenda kuwataarifu rasmi kuwa siku ya Simba Day, Simba Sports Club itacheza mechi na InterClube ya Angola  kwenye mechi hii wachezaji wetu wapya wataonekana rasmi baada ya maandalizi ya kutosha, kabla ya mechi hii kutakuwa na mechi kali ya utangulizi kati ya Simba Under 20 mechi hizi nina uhakika itakuwa burudani tosha.
Kama ambavyo mnajua Ubunifu ni jadi ya Simba tunatarajia kuwa na burudani mbalimbali ikiwamo wimbo maalum wa Simba, Wanamuziki nguli na Surprise kwa watazamaji watakaolipia kiingilio.
Kama ilivyokuwa mwaka jana Rais wa Simba atasaidiana na Kocha Mkuu wa Simba kwenye benchi la ufundi.
Ndugu wanahabari,
Kabla sijamaliza, napenda kuwashukuru sana kwa kuwa karibu na klabu yetu ya Simba. Matukio ya hivi karibuni na yatakayo kuja katika siku chache zijazo yanatosha kuwaambia na kudhihirisha lengo na dhamira ya Uongozi wangu wa kujenga timu imara sio  Tanzania tu, bali Afrika.
Nashukuru kwa kunisikiliza.




Katibu wa Simba Partick Kihemela akiongea

0 Responses to “JIANDAE KUWAONA INTERCLUBE SIKU YA SIMBA DAY ”

Post a Comment

More to Read