Tuesday, July 26, 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AITISHA MKUTANO NA VIONGOZI MBALIMBALI DODOMA



Ikiwa ni siku moja tangu Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa atangaze rasmi kuwa ofisi yake ifikapo mwezi Septemba itakuwa tayari imehamia Dodoma, Muda huu Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa, ameitisha mkutano kati yake na viongozi wakuu wa Mkoa wa Dodoma.




Wakuu wengine ambao wanakutana na Waziri Mkuu Majaliwa ni wote wanaotoka katika Taasisi za fedha, Siasa, Dini, Taasisi zote za Serikali  vikiwemo Vyuo Vikuu,  Wabunge wote wa mkoa wa Dodoma, Wakuu wa Wilaya zote, vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Mpaka sasa ukumbi wa mikutano uliyopo katika jengo la hazina ndogo, umekuwa mdogo kufuatia mwitiko mkubwa katika mkutano huo.
Wakati viongozi mbalimbali wakisubiri kuanza kwa mkutano huo, Mwendesha mkutano (MC) Peter Mavunde amewaambia viongozi hao kuwa kubwa wasubirie kupokea taarifa kuhusu uamuzi wa Serikali katika utekelezaji wake wa kuhamisha makao makuu yake mkoani humo.



Suala hilo liliamuriwa Machi 1973, wakazi wa mkoa wa Dodoma wakiwa 15,000 tu na sasa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa sasa hivi na Meya wa Mji wa Dodoma, Jafari Mwanyemba, katika mji  huo tu kuna wakazi 500,000
 


0 Responses to “WAZIRI MKUU MAJALIWA AITISHA MKUTANO NA VIONGOZI MBALIMBALI DODOMA ”

Post a Comment

More to Read