Wednesday, July 27, 2016
MTUHUMIWA WA KESI YA MILLION 7 KWA DAKIKA AFIKISHWA MAHAKAMANI
Do you like this story?
Mtuhumiwa wa kesi ya utakatishaji pesa wa Tsh Million 7 kwa Dakika
Bw Mohammed Yusuph Ally leo amepandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya
Hakimu mkazi Kisutu na mshikiwa mwenzake
Samweli Lema kwa mashitaka ya
kuhujumu uchumi wa Nchi.
Wakisomewa mashitaka yao na wakili wa
serikali Bw Kishemi Mutelemwa katika kesi namba
36 2016 ambapo jumla yao
wamekutwa na mashitaka 220 ya uhujumu uchumi ikiwa ni pamoja na kukwepa kulipa
kodi na kuitia hasara mamlaka ya mapato
Nchi (TRA) zaidi ya million 14
Kesi hiyo ambayo ilinguruma kwa
takribani masaa matatu imekuwa na mvutano wa hoja za kisheria
ambapo Wakili wa upande wa utetezi Bw Alex Mgongolwa amedai kuwa shitaka namba
221 linamapungufu makubwa ambayo hayawezi kurekenbishika hivyo amedai kufutilia
mbali shtaka hilo la utakatishaji fedha.
Kwa upande wa wakili wa upande wa
serikali Bw Kisheni Mutelemwa ameiomba mahakama
kuahirisha kesi hiyo mpaka 28
Julai, 2016 ili waweze kufatilia madai ya upande wa utetezi
Hakimu wa kesi hiyo Mh Willbad
Mashauri aliahirisha kesi hiyo mpaka siku ya alhamisi ya tarehe 28/7/2016
ambapo washtakiwa wamerudishwa tena rumande.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MTUHUMIWA WA KESI YA MILLION 7 KWA DAKIKA AFIKISHWA MAHAKAMANI ”
Post a Comment