Wednesday, July 27, 2016

KIKWETE: KASHFA YA KUIPENDELEA BAGAMOYO ILINIHUDHUNISHA SANA


Raisi mstaafu wa awamu ya 4 Mh Jakaya Kikwete amesema hakufurahishwa na mambo ambayo yalikuwa ni changamoto katika utendaji wake  wakati  hasa lile lakudaiwa kuwa alikuwa akiipendela kwao zaidi Bagamoyo.

Katika swala la kundeleza miradi ya maendeleao Raisi Kikwete amesema alikutwa na wakati mgumu pale ambapo alitaka kuendeleza miradi ya maendelo katika wilaya yake ya Bagamoyo na mkoa wa Pwani kwa ujumla kitu ambacho kilikuwa kikimnyima raha kwani baadhi ya vionngozi wakubwa wa serikali na wakuaminika  pamoja na baadhi ya wabunge walisema anaipendela Bagamoyo tu ilihali kuna maeneo mengine yanahitaji maendeleo
 


Raisi Kikwete alisema kuwa  kuna wakati alilazimika kuhamisha Fedha za  miradi ya Bagamoyo na kupeleka kwenye ujenzi wa maeneo ya  Geita, Sengerama hadi Usagara kipindi ambacho Waziri wa ujenzi alikuwa Mh Basil Mramba  lakini yote hayo hawakuyaona

“Hali kama hii ilikuwa inaninyima usingizi kwani siwezi kupeleka maendeleo sehemu niliyotoka tu, na swala la kuwanyima maendeleo nikitu ambacho hakiwezekani” alisema Kikwete  wakati wa sherehe za kupokelewa na kupewa pongezi kwa kukabizi kiti cha uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na kumaliza muda wake wa uongozi salama. 

Sherehe hizo  zilipambwa na ngoma za asili kutoka kabila la Wakwele na Wazaramo kutoka  wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
 


0 Responses to “KIKWETE: KASHFA YA KUIPENDELEA BAGAMOYO ILINIHUDHUNISHA SANA”

Post a Comment

More to Read