Wednesday, July 27, 2016
TENGENI NA KUSIMAMIA FEDHA KWA AJILI YA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE.MKUU WA MKOA WA MBEYA
Do you like this story?
Madiwani wakiwa Makini kupitia Hoja hizo. |
Viongozi kutoka Serikalini wakiwa wanawasilisha Hoja za Mkaguzi wa Mahesabu za Serikali mbele ya Mkuu wa Mkoa na Madiwani. |
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewataka madiwani wa halmashauri zote saba Mkoa
wa Mbeya kutenga na kusimamia upelekaji Fedha kwa vikundi vya Vijana na
wanawake kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na serikali.
Hayo ameyasema Leo wakati wa kikao na madiwani wa halmashauri ya Mbeya Dc wakati wa kujadili hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali.
Amewaambia halmashauri zinatenga Fedha asilimia 10 katika bajeti zao kwa ajili ya kusaidia vikundi vya Vijana na wanawake lakini inapokuja katika utekelezaji Fedha hizo hazipelekwi.
Hivyo amewataka halmashauri zote kutenga na kuzifuatilia Fedha hizo ziende kwenye vikundi na vikundi vitakavyopata hizo Fedha hizo vielezwe umuhimu wa urejeshaji wa fedha hizo kwa riba nafuu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TENGENI NA KUSIMAMIA FEDHA KWA AJILI YA KUWAWEZESHA VIJANA NA WANAWAKE.MKUU WA MKOA WA MBEYA”
Post a Comment