Wednesday, November 23, 2016
NEYMAR AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA
Do you like this story?
Mwendesha
mashitaka ya umma wa Hispania leo amefunga jalada la kesi iliyokuwa ikimkabili
mchezaji wa soka wa Barcelona Neymar kwa kutoa hukumu ya miaka miwili
jela baada ya kupatikana na hatia ya rushwa kwenye uhamisho wake kutoka klabu
ya Santos ya Brazil kwenda Barcelona mwaka 2013.
Jaji Jose Perals pia amemhukumu miaka mitano jela rais wa zamani wa Barcelona Sandro Rosell huku klabu ikipigwa faini ya Euro milioni 8.4 ($ 8,900,000). Jaji Jose pia amemwagiza rais wa sasa wa Barcelona Josep Maria Bartomeu kujiuzuru kisha afunguliwe mashitaka.
Kesi ya Neymar ilitokana na malalamiko ya kampuni ya uwekezaji ya Brazil (DIS), ambayo inamiliki asilimia 40 ya haki ya uhamisho wa Neymar ikidai kupokea pesa kidogo tofauti na maelewano huku ikiituhumu klabu ya Barcelona kuficha thamani halisi ya mkataba wa uhamisho wa Neymar.
Awali Barcelona walikubali kulipa faini ya kiasi cha Euro milioni 5.5 ($ 6,200,000) ili kufuta kesi hiyo ya ukwepaji kodi na hakimu Jose de la Mata alifuta jalada hilo mwezi Juni, kabla ya Mwendesha mashitaka ya Umma kupindua maamuzi hiyo na kuirudisha kesi mahakamani mwezi Septemba.
Kesi hiyo imekuwepo mahakamani tangu mwaka 2014 ambapo ilimlazimu rais Sandro Rosell kujiuzuru ili aweze kutoa ushahidi mahakamani sambamba na Bartomeu, Neymar na baba yake Neymar.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NEYMAR AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA”
Post a Comment