Sunday, November 27, 2016
SERIKALI YAMPOKONYA SUMAYE SHAMBA LAKE LENYE UKUBWA WA HEKTA 33
Do you like this story?
Waziri
Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amepokonywa na Serikali shamba lake lenye ukubwa
wa hekta 33 kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuliendeleza.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo
baada ya Sumaye kushindwa kuliendeleza kama notisi ya siku 90 ilivyoeleza.
“Oktoba
28, mwaka huu. Rais John Magufuli alibatilisha hati ya kumiliki ardhi ya shamba
namba 3074 lililopo Mabwepande. Shamba hili lilikuwa na hati namba 53086. Jina
la mmiliki lililoandikwa katika hati ni Frankline Sumaye,” amesema Hapi.
Sumaye
ambaye alikuwa ni mmoja wa wasemaji tegemeo katika mikutano ya kampeni ya
Uchaguzi Mkuu uliopita ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anamiliki
mashamba makubwa yaliyoko Morogoro na Mabwepande Dar es Salaam.
Baada
ya Rais Magufuli kubatilisha hati hiyo, Hapi amesema kuanzia sasa ni marufuku
kwa Sumaye kujihusisha na shamba hilo.
Kwa
sababu hati yake imeshabatilishwa na akibainika kufanya chochote vyombo vya
dola vitachukua nafasi yake.
“Vyombo
vya ulinzi na usalama watakuwapo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba shamba hili
halitafanyiwa shughuli zozote, isipokuwa baada ya taratibu za manispaa
zitakapofanyika,” amesisitiza Hapi.
Amesema
amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli
kupima viwanja vya shamba hilo na kwamba wananchi waliokuwa na mgogoro wa
shamba hilo wafikiriwe.
Februari
5 mwaka huu, akiwa Morogoro, Rais John Magufuli aliwataka watu wote
waliotelekeza mashamba kuyaendeleza, la sivyo atawanyang’anya na kuwapa
wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ SERIKALI YAMPOKONYA SUMAYE SHAMBA LAKE LENYE UKUBWA WA HEKTA 33”
Post a Comment