Sunday, November 27, 2016

MABADILIKO YALIYOFANYWA KWA VIONGOZI WA IDARA ZA TAKUKURU NA SABABU ZAKE




Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imefumua idara zake tatu kati ya tano, ikiwa ni pamoja na kumhamisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi.

Mabadiliko hayo yanafanyika ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu Rais John Magufuli alipomwondoa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athumani na kumteua kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

Nafasi ya DCI na ile ya Takukuru shughuli zake kwa kiasi kikubwa zinarandana, isipokuwa tu ile ya Takukuru imejikita kwenye rushwa wakati nafasi hiyo nyingine inahusu makosa ya kihalifu yote. Hivyo ni wazi kuwa mabadiliko hayo, kwa pamoja, yanalenga kusuka upya vyombo hivyo ili kukabiliana na wimbi la uhalifu linalokua kwa kasi.

Taarifa kutoka ndani ya Takukuru ambazo  zilisema mabadiliko hayo yamefanywa na Mkurugenzi Mkuu, Kamishna Valentino Mlowola, ikiwa sehemu ya kuboresha utendaji kazi.

Mabadiliko hayo yamewakumba Mkurugenzi wa Uchunguzi, Alex Mfungo, anayehamishwa kwenye kitengo hicho na kupelekwa kuwa Mkurugenzi wa  Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu. Na aliyekuwa akishika nafasi hiyo Ekwabi Mujungu, amepelekwa kuw Mkurungezi wa Elimu kwa Umma.

Aidha, Mbengwa Kasumambuto ambaye ni Mchunguzi Mkuu Makao Makuu, kwa mujibu wa taarifa tulipata sasa atakuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Taasisi hiyo. Na aliyekuwa Mkurugenzi wa Utafiti na Takwimu, Safina Seja ataendelea kuwa Mkurugenzi hapo hapo alipo, huku Kulthum Mansoor akibaki kwenye nafasi yake ya Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini.

Mabadiliko hayo yalifanywa siku ya alhamisi wiki hii na utekelezaji wake utaanza rasmi Alhamisi ya wiki ijayo. Na alipotafutwa msemaji mkuu wa Takukuru alithibitisha kuwepo kwa mabadiliko hayo huku akisema mabadiliko yamelenga kuongeza ufanisi wa utendaji kazi

0 Responses to “MABADILIKO YALIYOFANYWA KWA VIONGOZI WA IDARA ZA TAKUKURU NA SABABU ZAKE”

Post a Comment

More to Read