Monday, November 21, 2016

WAZIRI AAGIZA KUKAMATWA HARAKA KWA MAAFISA UVUVI




Waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Mh CharlesTizeba ametembelea soko la kimataifa la samaki Feri na kumwagiza katibu mkuu  wa wizara hiyo kuhakisha  maafisa uvuvi wote wanaoruhusu uingizwaji na uuzwaji wa samaki katika masoko mbalimbali nchini na hususani soko  hilo la kimataifa la samaki Feri wakamatwe na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria mara moja kwani  uvuvi wa mabomu umekuwa ukilidhalilisha taifa katika medali za kimataifa za uvuvi.

Mh Tizeba ameyasema hayo baada ya kutembelea soko hilo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mvuvi duniani novemba 21 na kuongeza kuwa uvuvi wakutumia mabomu umekuwa ukilidhalilisha taifa kwani nchi nyingi sasa hivyo hata zile za Afrika Mashariki hazifanyi hivyo tena.

Baadhi ya wavuvi waliokuwepo katika maadhimisho hayo wameelezea  changamoto wanazokutana nazo ikiwemo ukosefu wa vifaa vya  kisasa vya  uvuvi na hivyo kushindwa kuboresha uvuvi wao.

Awali waziri huyo alitembelea katika soko la kukaanga samaki na kuzungumza nao huku akionyesha wasiwasi kuhusu ubora wa mafuta yanayotumika kukangia mafuta hayo kama kweli yanabadilishwa  kwa wakati ambapo mwenyekiti wa wakaangaji hao  Bw. Ali  Mbonde alisema wanajitahidi kuhakisha yanabadilishwa.

0 Responses to “WAZIRI AAGIZA KUKAMATWA HARAKA KWA MAAFISA UVUVI”

Post a Comment

More to Read