Monday, November 21, 2016
MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) KUTUA MBEYA KWA UKAGUZI WA SOKO LA MWANJELWA.
Do you like this story?
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa
Hesanu za serikali(CAG), anatarajia kuanza kufanya kazi ya ukaguzi maalum
katika halmashauri ya Jiji la Mbeya baada ya kudaiwa kuwepo kwa viashiria vya
ubadhilifu wa fedha zilizotumika kukamilisha ujenzi wa soko la Mwanjelwa.
Awali, Agosti 9 mwaka huu, Waziri Mkuu Kassimu
Majaliwa akiwa katika ziara yake Mkoani Mbeya, alifanikiwa kutembelea mradi huo
wa soko ambao inasemekana umetumia kiasi cha shilingi Bilioni 26, tofauti na
matarajio ya serikali.
Serikali, ilikuwa ikiamini mradi huo utagharimu
kiasi cha shilingi bilioni 16 lakini kutokana na utendaji kazi wa hovyo
unaodaiwa kufanywa na baadhi ya watendaji tena kwa maslahi yao binafsi ulisababisha
soko hilo kutumia kiasi cha shilingi bilioni 26.
Hatua hiyo ndio iliyomfanya waziri Mkuu, kumuagiza
Mkaguzi Mkuu wa Hsabu za serikali kwenda Mbeya na kufanya ukaguzi wa mradi huo
ili kuondoa utata uliopo juu ya kiasi sahihi cha fedha kilichotumika kwenye
mradi huo.
Akizungumzia hilo, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya,
David Mwashilindi amesema kuwa baada ya agizo la waziri mkuu kutolewa,
halmashauri ilianza mchakato wa kumuita mkaguzi huyo ili kufika kufanya
ukaguzi.
Amesema, kinachofanyika sasa ni kamati ya fedha
kuketi kwa ajili ya kupitisha matumizi hayo ya fedha na kazi kuanza kufanyika
ikiwa na kutekeleza agizo la Waziri Mkuu.
Amesema Kamati ya fedha inataraji kukaa November 22
mwaka huu, na kutoa maamuzi na kupitisha kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya
kutumika kwa kazi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya kufanya ukaguzi wa
fedha katika soko la Mwanjelwa.
Aidha, Meya huyo aliwaomba wafanya biashara wote
ambao tayari waliingia mikataba na halmashauri ya Jiji, kuanza kuendesha
biashara zao kama makubaliano ya mkataba yanavyoelekeza.
Hata hivyo, aliongeza kuwa tayari halmashauri
imeingia mkataba na wakala atakayendesha zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara
wote ambao wamekiuka makubaliano ya mkataba kwa kushindwa kuendesha biashara
kwa kipindi husika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) KUTUA MBEYA KWA UKAGUZI WA SOKO LA MWANJELWA.”
Post a Comment