Friday, April 28, 2017

DKT MWAKYEMBE AKABIDHIWA TUZO NA RITA




Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini nchini (RITA), umempa Tuzo, aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe, kwa kutambua mchango wake katika kuboresha hali ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu nchini
Dkt Mwakyembe amekabidhiwa Tuzo hiyo na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, katika Ofisi za Wizara mjini Dodoma.

Kwa upande wa Profesa Kabudi, amempongeza Dkt Mwakyembe kwa jinsi alivyojitoa na kuhakikisha hali ya usajili inaboreshwa na hivyo kuinua muamko wa wananchi na kuona umuhimu wa kujisajili na kuwa na cheti cha kuzaliwa.

Kwa upande wake, Dkt. Mwakyembe baada ya kupokea Tuzo hiyo alisema “Sina neno kubwa la kuwaambia zaidi ya asante. Asanteni sana, niwaahidi kwamba nitaendelea kuwaunga mkono huko nilipokwenda. Nanyi lazima muendeleze kazi ya kuhamasisha usajili kwa nguvu zenu zote, na mjue kwamba mna kazi kubwa mbele yenu na ni lazima ifanikiwe.”

0 Responses to “ DKT MWAKYEMBE AKABIDHIWA TUZO NA RITA”

Post a Comment

More to Read