Wednesday, April 19, 2017
Mwanajeshi auawa kwa kuchomwa visu na vibaka
Do you like this story?
ASKARI
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), MT 94293, aliyefahamika kwa jina
la Tekeli Israel (29), ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani na watu
wanaodaiwa kuwa ni vibaka.
Akithibitisha
kuuawa kwa askari huyo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles
Mkumbo, alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa nne usiku, wakati
marehemu, ambaye ni mkazi wa Mbaunda, alipokuwa akitoka kula chips.
Alisema
marehemu wakati akitoka baa ya Tarakea kwenda nyumbani kwake, alipofika
eneo la Tarakea Super Car Wash, mtaa wa Simanjiro, kata ya Sombetini,
asikia kelele za mtu akiomba msaada.
Kamanda
Mkumbo alisema mtu aliyekuwa anapiga kelele za kuomba msaada
alifahamika kwa jina la Tumkislai Abdallah, ambaye alikuwa akiporwa simu
ya kiganjani na vibaka.
"Baada
ya marehemu kufika eneo la tukio na kubaini kuwa ni vibaka, aliamua
kupambana nao, lakini kwa bahati mbaya walimjeruhi kwa visu na mmoja wao
alimchoma nacho kifuani,"alisema.
Kwa
mujibu wa Kamanda Mkumbo, wananchi kwa kushirikiana na polisi,
walifanikiwa kumtia mbaroni kibaka mmoja, aliyefahamika kwa jina la
Dickson Moses(19), maarufu kwa jina la 'Tukai', mkazi wa Olmatejoo,
ambaye alimchoma kisu marehemu.
Alisema
baada ya mtuhumiwa kuhojiwa na polisi, aliwataja wenzake watatu, ambao
walifanikiwa kutoroka na kwamba, polisi wanawasaka popote pale walipo.
"Jeshi
la Polisi mkoa wa Arusha linawataka watuhumiwa watatu, ambao majina yao
tunayo, waliokuwa na Tukai kwenye tukio la mauaji ya mwanajeshi huyo,
kujisalimisha mara moja kwani mkono wa serikali ni mrefu utawatia
nguvuni popote pale walipo," alisisitiza.
Mmoja
wa mashuhuda wa tukio hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Ally Omaiy,
alisema walimuona marehemu kwenye baa ya Tarakea, ambako alikula chispi
kisha akaondoka.
Alisema
dakika chache baadaye, walisikia kelele za mtu anaomba msaada na baada
ya kufika eneo la tukio, walimkuta marehemu akipambana na vibaka hao na
ghafla walimuona ameanguka chini.
Alisema
baada ya kuanguka, vibaka hao walianza kukimbia, lakini wananchi kwa
kushirikiana na madereva wa bodaboda, waliwakimbiza na kufanikiwa
kumkamata mmoja wao.
"Marehemu
alipambana na vibaka hao kwa ajili ya kumsaidia Abdallah asiporwe simu,
lakini kwa kuwa vibaka walikuwa wanne, walimzidi nguvu na mmoja
alifanikiwa kumchoma marehemu kisu cha kifuani na kufariki dunia," alisema.
Shuhuda
mwingine, ambaye ni rafiki wa karibu wa marehemu (Jina linahifadhiwa),
alisema marehemu alikuwa anajiandaa kwa ajili ya safari ya kwenda
Darfur.
"Marehemu
alikuwa rafiki yangu wa karibu, tunaishi jirani hapa Mbauda,
tulishirikiana kwa mambo mengi, licha ya mimi kuwa raia wa kawaida na
aliniambia ameshakamilisha taratibu zote za kikosini na kwamba, alikuwa
anajiandaa kwa ajili ya kwenda Darfur," alisema.
Mwili
wa marehemu Israel, umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti
katika Hosptali ya Mkoa ya Mount Meru, ukisubiri taratibu za
kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Mbeya kwa maziko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)

