Saturday, May 27, 2017
Habari Mpya kutoka kwa Meya wa Jiji la Dar Es Salaam
Do you like this story?
MSTAHIKI
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita , jana amezindua mashindano
ya ngumi ya kombe la mstahiki Meya na kusisitiza kuwa kuna kila sababu
ya kutoa kipaumbele kwenye mchezo huo ili uweze kuwa ajira sambamba na
kuibua vipaji kwa vijana.
Meya
Mwita alisema kuwa michezo ni afya na kwamba atajitoa kadiri ya uwezo
wake ili kufanikisha mchezo huo kuwa chanzo cha ajira kama ilivyokuwa
kwenye nchi za nje.
Alifafanua
kuwa nchi nyingine wapo watu walioajiriwa kupitia mchezo huo na kwamba
hata hapa kwetu uwezo huo upo lakini kinachotakiwa ni kujitoa na
kuthamiria kuwekeza nguvu kubwa kwenye mchezo huo.
“
Mchezo ni afya, leo hii nimefarijika sana kuona vijana wengi
waliojitokeza kushiriki mpambano huu, kutokana na hilo kama meya wa jiji
hili, na mdhamini mkuu wa mashindao haya, nitakuwa pamoja na nyinyi”
alisema Meya Mwita.
Akizungumzia
changamoto zilizotolewa na Mwenyekiti wa chama cha ngumi mkoa wa Dar es
Salaam, Carol Godfrey , Meya mwita alisema atasaidia kutoa vifaa vya
michezo huku changamoto ya uwanja akiahidi kulishughulikia.
Aliongeza
kwamba kwakuwa anahitaji maendeleo ya mchezo wa ngumi, atahakikisha
kuwa kwa nafasi aliyokuwa nayo anawawezesha wachezaji ikiwa ni lengo la
kuhamasisha vijana wengi wenye vipaji vya mchezo huo kujitokeza.
“
Najua wapo vijana ambao wanavipaji wa mchezo huu, lakini bila
kuwezeshwa hatuwezi kuwapata wala kusonga mbele, sasa niweke akiba ya
maneno, lakini nitalisimamia” aliongeza.
Akizungumzia
mashindano hayo, Meya Mwita alisema kuwa waamuzi wa mchezo huo (Marefa)
wanapaswa kutenda haki bila kuwepo hali ya hujuma na kwamba
anayestahili kupata tuzo hiyo ndio apatiwe.
Alisema
wapo baadhi ya waamuzi wa michezo mbalimbali sio waminifu na kwamba
wamekuwa na tabia ya kupanga matokeo , hivyo akaonya kwa kusisitiza kuwa
jambo hilo kwenye mashinda hayo lisijitokeze.
“
Waamuzi naomba muwe waminifu, ili muweze kujenga imani kwa watu ambao
mko nao hapa, jambo la kupanga matokeo sio zuri, hivyo aliyestahili
kushinda ndio apewe nafasi hiyo nasio kupindisha matokeo” alisema Meya
Mwita.
Hata
hivyo katika hatua nyingine aliwataka wachezaji wote walioshiriki
michuano hiyo, kuzingatia sheria na kuwaheshimu walimu wanaowafundisha
ili kujenga nidhamu bora ya mchezo huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)