Saturday, May 27, 2017
Mbunge wa CHADEMA achukizwa na neno Bwege alilolisema Zungu
Do you like this story?
Mbunge
wa Tarime Mjini (Chadema), Ester Matiko juzi jioni alikerwa na ujumbe
unaodaiwa kuandikwa na Mwenyekiti wa Bunge, Musa Zungu uliowataka
wapinzani waache mambo ya kibwege.
Matiko
ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, aliomba mwongozo wa
Spika mara baada ya Bunge kupitisha bajeti ya wizara hiyo.
Matiko
aliomba mwongozo huo akitaka kupata ufafanuzi wa utaratibu unaotumika
kuwachagua wabunge watakaohoji wakati Bunge linapokaa kama kamati.
Alisema
katika Bunge la 11 umekuwa utaratibu wa kiti cha Spika kuchagua wabunge
wengi wa CCM kuchangia hoja na hivyo muda kumalizika bila wapinzani
kupata nafasi.
Mbunge
huyo alisema jambo hilo limekuwa tofauti na mabunge mengine ambayo
Bunge limekuwa likienda hadi saa nne usiku ili kuwapa nafasi wabunge
kujadili bajeti kwa kina.
“Tukikulalamikia
matokeo yake unatutumia kikaratasi kimeandikwa maneno, mambo yenu ya
kibwege bwege. Yaani unawaambia wananchi wa Tarime wamechagua bwege?”
alihoji Matiko.
Akijibu mwongozo huo, Zungu alisema kanuni zinatoa fursa ya kuingia katika kupitisha vifungu kwa utaratibu wa fungu.
Alisema
kanuni hiyo pia inatoa fursa ya vyama kupeleka majina ya wachangiaji
katika kila kamati ya matumizi inapokaa kupitia bajeti.
Aliwataja
waliowasishwa kwa ajili ya bajeti hiyo kuwa ni ni Matiko, Chacha Rioba
(Serengeti) na mbunge mwingine wa tatu ambaye hakumtaja jina. “Unasema
sijui kuna karatasi mimi nimesema, hiyo karatasi iangalie vizuri imetoka
wapi? Sasa wewe unaweza ukaichukua hiyo karatasi ukaipeleka kwa katibu
ili ifanyiwe kazi,” alisema Zungu.
Majibu hayo yalisababisha minong’ono miongoni mwa wabunge, lakini Zungu alisema kuwa mwongozo ni huo na kuliahirisha Bunge.
Akizungumza
jana kuhusu suala hilo, Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya
alisema inapofika Bunge linapokaa kama kamati ya matumizi kila chama
kimekuwa kikitakiwa kupeleka majina ya wachangiaji.
Alisema
kuna wakati hoja moja wanapewa wabunge hata 10 kuchangia na kwamba hata
kama ni uamuzi wa kiti lakini ni lazima busara itumike.
“Wanafanya hivyo ili kuhakikisha kuwa upinzani unakosa nafasi na hiyo tumekuwa tukilalamika hata kwa Zungu,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)