Thursday, June 1, 2017
Alichosema Lowassa baada ya Kifo cha Ndesamburo
Do you like this story?
Mjumbe
wa Kamati ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward
Lowassa ameeleza kusikitishwa na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Moshi
Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema) na kueleza kuwa alikua shujaa wa
mabadiliko.
Lowassa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter ametweet, “Nimesikitishwa
sana na kifo cha ghafla cha Mzee Ndesamburo, Mungu ailaze roho yake
mahala pema peponi natoa pole kwa familia na wote. Mzee Ndesamburo
alikua shujaa wa kweli wa mabadiliko wa miaka mingi na mwenye mchango
mkubwa kwenye siasa za demokrasia katika Taifa letu
Ndesamburo
aliyekuwa Mbunge kuanzia mwaka 2000 hadi 2015 amefariki dunia ghafla wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi
mkoani Kilimanjaro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)