Monday, October 23, 2017

MARIE STOPES LAUNCHES MWENGE CALL CENTRE




 Marie Stopes Tanzania (MST) re-opened its newly refurbished Mwenge Hospital located at Plot number 421 & 422, Kinyonga Street in Kijitonyama, Dar es Salaam.

Speaking during the re-launch event, The Danish ambassador to Tanzania, H.E. Einar HebogĂ„rd Jensen who presided over the event, commended MST for complementing the Government of Tanzania’s efforts in ensuring that all citizens have access to quality health services at affordable costs.

“In Tanzania, Marie Stopes is very well known for providing quality healthcare services which are affordable to most of Tanzanians, greatly complementing the Government of Tanzania’s efforts,” Mr. Jensen pointed out.

The refurbishment of the hospital has been a fruitful product of exciting collaborative efforts between MST and DANIDA/ Embassy of Denmark thereby making the hospital a one-stop health facility for family planning and sexual reproductive health services.

He said the partnership between DANIDA and Marie Stopes would be continuous for the benefit of all Tanzanians.



“We will continue to invest within the communities that we operate in as a way of supporting our key projects such as Health, Education and Poverty eradication.”

Mr. Jensen also launched the MST Contact (Call) Centre along with a toll free customer care number that will give the public the opportunity to inquire on MST services at no cost.

Maries Stopes Tanzania Country Director, Anil Tambay delivers his speech during the event.

On his part, The Country Director for Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay said the refurbished hospital provides comfortability and a conducive environment for the sick.

With funding from DFID, DANIDA, and USAID, MST is implementing multiple projects supporting delivery of integrated family planning outreach services and other sexual reproductive health services, including comprehensive post abortion care (CPAC) and Gender Based Violence (GBV) initiatives. These projects are focused on improving access to sexual reproductive health information and services to needy communities throughout Tanzania.


Aside from the launch, MST Mwenge hospital has also commenced its three-days special campaign which aims at providing free Blood Pressure (PB) check-ups, Blood Sugar check-ups (RBG), HIV testing, provision of family planning services, as well as cervical cancer screening to visiting clients – while other general medical services will continue to be offered at a fee within the hospital.

Nationwide, MST provides Sexual & Reproductive Health services at scale, covering all regions in Tanzania through mobile family planning outreach services. In addition, general medical services are also provided at MST’s health centres. MST works very closely with the Government of Tanzania at all levels, supporting implementation of the fourth Health Sector Strategic Plan- HSSP-IV (2015 – 2020), as a public private partnership (PPP). In 2016, MST hosted almost 7 million client visits and delivered over 2.1 million Couple Years of Protection (CYP).

4:02 PM by fahari news · 0

Friday, September 15, 2017

UNICEF YAUPONGEZA UONGOZI WA MKOA WA MBEYA KWA USHIRIKIANO NA USIMAMIZI WA MIRADI



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Amosi Mkalla  azindua mradi wa mpango wa Afya na ujasiriamali kwa vijana





Picha ya Pamoja

Picha ya Pamoja



UONGOZI wa unicef umeupongeza uongozi wa Mkoa was Mbeya chini ya Mkuu wa mkoa kwa ushirikiano mkubwa wanaoupata ktk kutekeleza majukumu yao

 hayo yamesemwa  na mwakilishi wa unicef Bi Ulrike Gilbert Nandra Mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya katika   uzinduzi mradi wa mpango wa Afya na ujasiriamali vijana uliofanyika  katika Ukumbi wa Mkapa ukiendeshwa kwa pamoja kati ya Unicef na TASAF.

Mkuu wa mkoa ameipongeza unicef kwa misaada mingi katika sekta mbalimbali na amehaidi kusimamia kwa karibu miradi yote inayofadhiliwa na unicef

3:45 PM by fahari news · 0

WATU WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI MBEYA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA
Mwonekano wa Gari aina ya Coaster iliyopata ajali.




                                                       

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 15.09.2017.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaongeza jitihada za kuzuia na kupunguza matukio ya ajali za barabarani kwa kuhakikisha madereva na watumiaji wengine wa barabara wanafuata sheria na alama za usalama Barabarani. Aidha kumekuwa na ajali 01 ya vifo kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 14.09.2017 majira ya saa 19:45 usiku huko eneo la Mlima Iwambi, Kata ya Songwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya kwenda Tunduma, kulitokea ajali iliyohusisha magari matano yenye namba za usajili T. 231 BME aina ya Tipper ikiendeshwa na dereva FRED MWAKALINGA [33] Mkazi wa Itiji - Mbeya ikitokea Mbeya mjini kwenda Mbalizi, Gari yenye namba za usajili T. 515 ARE aina ya Fuso iliyokuwa ikiendeshwa na dereva EMMANUEL JULIUS [29] Mkazi wa Itiji ikitokea Mbalizi kwenda Mbeya mjini, Gari yenye namba za usajili T.126 DJZ aina ya Fuso basi iliyokuwa ikiendeshwa na AMOS MWAIKAJA @ CHODO [40] Mkazi wa Kagera – Soweto, Gari yenye namba za usajili BCA 8730 na tela BCA 8733 ikiendeshwa na EVANS MUSONDA [39] raia wa Zambia na Gari yenye namba za usajili T.570 CKC aina ya Toyota dyana ikiendeshwa na dereva AMOS BENSON pamoja na Pikipiki moja ambayo haijafahamika namba zake za usajili ikiendeshwa na dereva aitwaye JANIA JACKOBO @ SANGA [27] Mkazi wa Iwambi.

Katika ajali hiyo watu wanne walifariki dunia ambao ni dereva wa Gari yenye namba za usajili T.570 CKC AMOS BENSON, mwendesha Pikipiki ambayo bado hajafahamika namba zake za usajili aitwaye JANIA JACKOBO @ SANGA [27] Mkazi wa Iwambi, dereva wa Gari lenye namba za usajili BCA 8730/BCA 8733 EVANS MUSONDA [39] raia wa Zambia na Mwanamke mmoja ambaye bado hajafahamika ambaye alikuwa abiria kwenye Gari yenye namba za usajili T.570 CKC Toyota Dyana.

Aidha katika ajali hiyo, watu wengine tisa walijeruhiwa kati yao wanaume ni wanne na wanawake watano. Aidha kati ya majeruhi hao, wawili wamelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na saba wamelazwa Hospitali Teule Ifisi - Mbalizi. Chanzo cha ajali kinachunguzwa hata hivyo inahisiwa kuwa dereva wa lori alikosa umakini na kuanza kugonga magari mengine ambaye pia amepoteza maisha katika ajali hiyo. Upelelezi unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha ajali na dereva aliyehusika.

WITO:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa Madereva kuwa makini wanapotumia vyombo ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha Kamanda MPINGA anawataka madereva kufuata, kuheshimu na kuzingatia sheria na alama za barabarani ili kuepuka ajali.

                                              Imesainiwa na:
 [MOHAMMED R. MPINGA - DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

1:43 PM by fahari news · 0

More to Read